Ajitokeza kufukua kaburi la Kiyeyeu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,871
155,839

Siku kadhaa baada ya kuripotiwa taarifa za Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), mkoani Iringa kushindwa kuhamisha kaburi la Martin Kiyeyeu kwa ajili ya kupisha ujenzi wa barabara kutokana na imani za kishirikina, mkazi wa Mafinga Sadick Mhomanzi, amesema anaweza kufanya kazi hiyo kwa muda mfupi tena bila gharama kubwa.

Kaburi la Kiyeyeu linakadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 50 sasa lipo katika kitongoji cha Isimila, Kijiji cha Ugwachanya, wilayani Iringa karibu na barabara kuu ya Iringa kwenda Mbeya likiwa na historia ndefu kutokana na kushindikana kuondolewa katika eneo hilo mara kadhaa kutokana na miujiza iliyopo katika eneo hilo

Moja ya vituko vya kaburi hilo ni kushindikana kwa umeme kupita juu ya kaburi na pia linadaiwa kushindikana mara mbili kulitoa na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyeuawa kwa nyuki na mwingine kufariki ghafla akiendesha tingatinga kulitoa kaburi hilo.

Akizungumza na chanzo chetu cha habari Mhomanzi alisema kaburi hilo linaweza kuondolewa bila madhara yeyote tofauti na maelezo ya watu kwamba watu kadhaa wameshapoteza maisha kwa kujaribu kufanya hivyo.

Mhomanzi alitoa kauli hiyo wakati ambapo taarifa za uhakika kutoka katika eneo la kijiji hicho zikidai juhudi za kuliondoa kaburi hilo ili kupitisha barabara eneo hilo zimekuwa zikishindikana hata pale ilipotumika familia ya Marehemu Martin Kiyeyeu mwenyewe.

Lakini Mhomanzi kwa kujiamini alisema atakwenda yeye mwenyewe na kutumia jembe lake la mikono kuchimba na kuondoa udongo huo hadi mifupa ya marehemu Kiyeyeu na kuihamisha bila ya kudhurika. "Amini maneno yangu kuona kaburi linashindikana kuondolewa, hakuna mtu anayeweza kushindwa, kaka mimi niko tayari nitafanya kazi hiyo kwa mkono wangu kabisa,"alisema Mhomanzi.

Mhomanzi alihoji "Kama ndugu wa marehemu wameridhia kuondolewa kwa kaburi hilo na kupatiwa eneo mbadala ni kitu gani kinaweza kuzuia? mimi siamini hivyo,Tanrods waniwezeshe mimi kuifanya kazi hiyo, nitakwenda na jembe langu pamoja na koleo kuifanya kazi hiyo nitakachokosa ni trekta la kubebea udongo na mifupa"alisema .
 
Sipati picha, miaka na miaka kaburi limegoma kung'oka halafu lije ling'olewe leo?
Huyo atakaye ling'oa hilo kaburi ninamuahid shilingi laki 2.
 
Hospitali hazina dawa, yatima hawana nguo wala chakula, wewe unataka kumwaga mahela kwa kuwapa wachawi???
Hebu waza mara mbili ndugu yangu
 
Hayo ni mawazo yako, kwani unajua ni jinsi gani nimekuwa nikijitolea kusaidia jamii?
Acha kukurupuka
 
nilipita hapo juz jtatu na kukuta watu kibao na magari yamepak hapo tanangoz wanaaangala kaburi hilo............kumbe walikuwa ni tanroad

miaka ile nasoma tosa kuna fuso moja ililipamamia kabuli hilo....cha ajabu hata rangi haikubanduka ila fuso ilikuwa imeharibika vibaya

shauri yake huyo jamaa...........
 
Ni vizuri tanroad wakakwepesha barabara kama walivyofanya kipindi cha nyuma kuepusha madhara zaidi, ila nashauri viongozi waweke utaratibu wa kuweka vivutio vya watalii wa ndani na nje ktk maeneo kama hayo na nadhani yako mengi hapa tz
 
hivi sababu ya hilo kaburi kudon't ni nini hasa.....naombeni mnieleweshe maana hainiingii akilini hii
 
Siku kadhaa baada ya kuripotiwa taarifa za Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), mkoani Iringa kushindwa kuhamisha kaburi la Martin Kiyeyeu kwa ajili ya kupisha ujenzi wa barabara kutokana na imani za kishirikina, mkazi wa Mafinga Sadick Mhomanzi, amesema anaweza kufanya kazi hiyo kwa muda mfupi tena bila gharama kubwa.

Kaburi la Kiyeyeu linakadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 50 sasa lipo katika kitongoji cha Isimila, Kijiji cha Ugwachanya, wilayani Iringa karibu na barabara kuu ya Iringa kwenda Mbeya likiwa na historia ndefu kutokana na kushindikana kuondolewa katika eneo hilo mara kadhaa kutokana na miujiza iliyopo katika eneo hilo

Moja ya vituko vya kaburi hilo ni kushindikana kwa umeme kupita juu ya kaburi na pia linadaiwa kushindikana mara mbili kulitoa na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyeuawa kwa nyuki na mwingine kufariki ghafla akiendesha tingatinga kulitoa kaburi hilo.

Akizungumza na chanzo chetu cha habari Mhomanzi alisema kaburi hilo linaweza kuondolewa bila madhara yeyote tofauti na maelezo ya watu kwamba watu kadhaa wameshapoteza maisha kwa kujaribu kufanya hivyo.

Mhomanzi alitoa kauli hiyo wakati ambapo taarifa za uhakika kutoka katika eneo la kijiji hicho zikidai juhudi za kuliondoa kaburi hilo ili kupitisha barabara eneo hilo zimekuwa zikishindikana hata pale ilipotumika familia ya Marehemu Martin Kiyeyeu mwenyewe.

Lakini Mhomanzi kwa kujiamini alisema atakwenda yeye mwenyewe na kutumia jembe lake la mikono kuchimba na kuondoa udongo huo hadi mifupa ya marehemu Kiyeyeu na kuihamisha bila ya kudhurika. "Amini maneno yangu kuona kaburi linashindikana kuondolewa, hakuna mtu anayeweza kushindwa, kaka mimi niko tayari nitafanya kazi hiyo kwa mkono wangu kabisa,"alisema Mhomanzi.

Mhomanzi alihoji "Kama ndugu wa marehemu wameridhia kuondolewa kwa kaburi hilo na kupatiwa eneo mbadala ni kitu gani kinaweza kuzuia? mimi siamini hivyo,Tanrods waniwezeshe mimi kuifanya kazi hiyo, nitakwenda na jembe langu pamoja na koleo kuifanya kazi hiyo nitakachokosa ni trekta la kubebea udongo na mifupa"alisema .

Kama huyo mtu ni mtaalam wa hayo mambo alete quotation yake hapa tutamlipa pesa yoyote kama anaweza kumpiga juju na kuondoa uhai wa Rostam Aziz, maana huyu mtu sasa amekuwa ni janga la taifa.
 
huyo mwongo tu anatafuta pesa yakula tu kwanini kumsumbua marehemu wakati kunawalio hai ambao ni majanga yataifa aje a2 rip
 
Wanyalu huyo mtu wenu mtampoteza! mwambieni kama anawatoto wadogo awalee kwanza ndo aanze kucheza na mambo hayo!

Ila mzee akifanikisha kulihamisha atajizolea umarufu yeye atakuwa ndo kivutio cha utalii.
 
nilipita hapo juz jtatu na kukuta watu kibao na magari yamepak hapo tanangoz wanaaangala kaburi hilo............kumbe walikuwa ni tanroad

miaka ile nasoma tosa kuna fuso moja ililipamamia kabuli hilo....cha ajabu hata rangi haikubanduka ila fuso ilikuwa imeharibika vibaya

shauri yake huyo jamaa...........

Tosa ulikuwa miaka ipi?
 
Kama huyo mtu ni mtaalam wa hayo mambo alete quotation yake hapa tutamlipa pesa yoyote kama anaweza kumpiga juju na kuondoa uhai wa Rostam Aziz, maana huyu mtu sasa amekuwa ni janga la taifa.

R.A amekukosea nini, nikipi alichomyanganya kwako: kauli yako niya kulea uzembe na ubinafsi wa wataalam wetu tunaowatuma kusaini mikataba na wawekezaji wakaamua kukamua 10% na kuiachia nchi madeni. Hawa ndo wakuanza kuwajibishwa kabla hujatangaza zabuni ya kigagura.
 
Hii nchi kila mtu anafikiria kula kiulani. Watu hawana malengo thabiti ya kuleta maendeleo.
hebu muone huyu Kigagura anataka alipwe kwanza. Kama yeye ana uwezo wa kuling'oa hilo kaburi kwanini asiombe asongewe ugali mkubwa kisha aanze kazi yake?
Baada ya hapo alipwe ujira wake
 
R.A amekukosea nini, nikipi alichomyanganya kwako: kauli yako niya kulea uzembe na ubinafsi wa wataalam wetu tunaowatuma kusaini mikataba na wawekezaji wakaamua kukamua 10% na kuiachia nchi madeni. Hawa ndo wakuanza kuwajibishwa kabla hujatangaza zabuni ya kigagura.

Sio kosa lako, hilo ndio tatizo la kutumia tumbo kufikiri badala ya kutumia ubongo. na bila shaka utakuwa unatokea igunga kule, mkichinjiwa ng'ombe watatu basi mnampa ubunge, pumbavu kabisa.
 
Hilo kaburi kuna gharama ngapi kulipisha libaki kama lilivyo? Wenzetu wanapisha hata makazi ya popo sisi tunashindwa kutambua asili na tamaduni za watu? Kama mwenye kaburi mwenyewe (kiyeyeu) angependa kuhamishwa kusingekuwa na longolongo zozote! Maendeleo tunayataka, lakini si kwa kusakrifaisi kacha na kusumbua waliolala, ardhi tunayo ya kutoshajamani!
Mimi nashauri kiyeyeu aachwe, tena ningekuwa mmoja wa wanafamilia ningeshika bango hasa. Mwacheni apumzike mzee wa watu, tangazeni maajabu yanayoonekana hapo na iwe ehemu ya utalii kama Nyumbanitu pale kibena-njombe, au kwa Mwanamalundi pale seke-shinyanga,Tomb of the Virgin, Tomb of David.
 
Back
Top Bottom