Ajitoa uhai kwa simanzi ya kumkumbuka mkewe

rpg

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Posts
3,620
Reaction score
1,480
Richard Kijazi, mkazi wa jijini Dar es Salaam, amejinyonga huku akiacha ujumbe unaodai kuwa amemkumbuka mkewe aliyefariki dunia. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema kuwa mwanaume huyo alikutwa amejinyonga chooni juzi saa 10:00 jioni maeneo ya Kijichi huku akiwa ameacha ujumbe wa maandishi mezani ambao sehemu yake inasomeka:

“Naomba nieleweke wazi kwamba tukio hili hajahusika mtu yeyote, ila nimeamua kufanya hivi kwa kuwa nimemmiss mke wangu, mama John. Naomba nizikwe Dar es Salaam na Mchungaji Haule, na ujumbe huu uheshimiwe”

Kwa mujibu wa kamanda, uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa mwaka 2012, Kijazi aliondokewa na mkewe wa ndoa, mama John kwa ugonjwa wa malaria. Alisema kuwa tangu wakati huo, tafrani ya kutishia kujinyonga ilianza mara kwa mara, lakini alikuwa akishindwa kutokana na msaada wa karibu katoka kwa ndugu zake.

Source: Wavuti
 
Niliisoma hii habari kwenye gazeti la jana, iliniuma sana! Hivi, ni mapenzi tu ya mkewe Mama John ndo yalisababisha amfuate au kuna kingine nyuma ya mapenzi ya Marehemu Mama John? Na hata hjamfikiria John atabaki katika mazingira gani baada ya baba na mama John kuondoka duniani.

Pole sana John, maana sasa do unakuwa mkiwa kamili, yatima.

Kwa Baba John Mungu ndo anajua kwa kukuweka hata kama utazikwa na TB Joshua!
 
Kwa Baba John M
ungu ndo anajua kwa kukuweka hata kama utazikwa na TB Joshua!

so sad!!!! akakae alipopachagua why umemchagua tb joshua?
 
Amani yake ilikuwa azikwe na Mchungaji Haule nikaandika kuwa hata ikiwa na TB Joshua, ni Mungu pekee anajua wapi atakaa.
 
duu

I wish Mama John angejua.

R.I.P mama na baba Joniii
 
Niliisoma hii habari kwenye gazeti la jana, iliniuma sana! Hivi, ni mapenzi tu ya mkewe Mama John ndo yalisababisha amfuate au kuna kingine nyuma ya mapenzi ya Marehemu Mama John? Na hata hjamfikiria John atabaki katika mazingira gani baada ya baba na mama John kuondoka duniani.

Pole sana John, maana sasa do unakuwa mkiwa kamili, yatima.

Kwa Baba John Mungu ndo anajua kwa kukuweka hata kama utazikwa na TB Joshua!

Mara nyingi baada ya kuondokewa na wapendwa wetu huwa tunakosa msaada stahiki wa kihisia,hii huwa inapelekea wengine kuwa depressed na mwisho wa siku kuchukua maamuzi kama hayo!
Inasikitisha ila ni jukumu la wanafamilia sasa kusaidia watu kama hawa wapate msaada kabla madhara kama haya hayajatokea!!
John masikini amebaki yatima.
 
Ennie ninakubaliana na wewe, lakini mama john alifariki mwaka 2012, inamaana baba john alikuwa hajapata repair ya kisaikolojia? Au pengo la mama john ni zaidi ya penzi?

Namuonea huruma John ambaye baba kaamua kumfuata mama wakati pengine huenda mama john aliacha wosia kwa baba john kuwa amtunze john.
 
Last edited by a moderator:

Inawezekana kabisa akawa hajapona kihisia mpaka leo.
Najua ninachokiongea MESTOD, nilifiwa na mume mwaka huo pia,najua nilivyovurugika kihisia na nilikopitia mpaka kuwa nilivyo leo.
Sim support huyo baba ila simshangai pia,jamaa zake walipaswa wamtafutie msaada alipoanza kutishia kujinyonga.
Viongozi wa dini wanamsaada sana kwenye hili.
 
Last edited by a moderator:
pole Ennie..
you are strong

Nijuavyo mimi muda ni tiba nzuri sana. Kwa muda huo ulopita sidhani kama unaweza chukua uamuzi wa kujitoa uhai leo (Pole sana kwa hili, Mungu azidi kukuimarisha). Katika hali yoyote ile, muda huo ulitosha kabisa kumpa tiba. Vinginevyo isiwe analimiss penzi la mama john tu, kuwe na sababu nyingine pia.
 
Muda ni tiba nzuri sana kama tu ukiukubali ukweli kuwa ameenda,hatorudi na maisha yanapaswa yaendelee bila uwepo wake.
Ukipingana na ukweli itakusumbua sana!!
Shukran!
 
Back
Top Bottom