Kutokana na urasimu, ubadhilifu na utapeli uliojitokeza katika mchakato wa kuajiri nguvu kazi katika idara ya uhamiaji, imebainika dhahiri kwamba hata utendaji kazi wao ungefanana moja kwa moja na yale yaliyojitokeza katika kupatikana kwao.
Kamati ndogo iliyoundwa ilipendekeza mchakato wa ajira hizo ufanywe na wizara. Hata hivyo, hiyo imeonekana sio suluhisho bali ni kuongeza tatizo kwani viongozi wengi wa wizara pia wanna ndugu na jamaa zao ambao wanatamani waajiriwe katika idara hiyo.
Pamoja na hayo, idara husika ya uhamiaji ipo chini ya wizara hivyo viongozi na mambo huenda yakawa yaleyale. Ili kuepusha yote hayo, imependekezwa kuwa ajira hizo zipelekwe kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwani kuna wengi wenye sifa na uwezo mkubwa wa kufanya shughuli hizo.