Ajira za uhamiaji zapelekwa JKT

Ajira za uhamiaji zapelekwa JKT

Kutokana na urasimu, ubadhilifu na utapeli uliojitokeza katika mchakato wa kuajiri nguvu kazi katika idara ya uhamiaji, imebainika dhahiri kwamba hata utendaji kazi wao ungefanana moja kwa moja na yale yaliyojitokeza katika kupatikana kwao.

Kamati ndogo iliyoundwa ilipendekeza mchakato wa ajira hizo ufanywe na wizara. Hata hivyo, hiyo imeonekana sio suluhisho bali ni kuongeza tatizo kwani viongozi wengi wa wizara pia wanna ndugu na jamaa zao ambao wanatamani waajiriwe katika idara hiyo.

Pamoja na hayo, idara husika ya uhamiaji ipo chini ya wizara hivyo viongozi na mambo huenda yakawa yaleyale. Ili kuepusha yote hayo, imependekezwa kuwa ajira hizo zipelekwe kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwani kuna wengi wenye sifa na uwezo mkubwa wa kufanya shughuli hizo.

Upuuzi wa hali ya juu. Hilo ndiyo suluhisho? Tutafanyaje ajira zitakazotokea kwenye mawizara mengine?

Dawa ilikuwa moja tu, kuwwajibisha wale waliofanya huo mchezo bila huruma. Hilo litakuwa somo kwa wizara zote.
 
....ni upuuzi ambao yapaswa WANANCHI tuwaamulie kweli hawa watu... Hakuna UHALALI wakuchukua wafanyakazi ambao tayari wapo kwenye AJIRA tena Jeshini halafu huku URAIANI wanaachwa wasomi pia kisa eti Kuogopa UNDUGU.
 
.....Haya Mambo ndiyo Chanzo cha Kupelekea VIJANA tuliowengi KUTAMANI kuzamia nchi za NG'AMBO hata kama ni Msomi au si Msomi ilimradi kutafuta UNAFUU wa maisha...

Bongo_Tz hapa USIASA siasa mwingi, Blaah blaaah za kila namna kupitia miamvuli ya TUME ziundwazo kila kukicha baada ya MIZENGWE kubainika mpaka URAIANI...
 
Aisee kama mtu alikuwa kapata kihalali halafu mambo yenyewe yanakuwa havi ndo ukisikia gundu inakuwa hivyo,ndio maana nchi hii mtu akikupa kazi ya kuhubiri uzalendo anakuwa anakutukana kabisa manake naamini kuna watu wangekuwa na uwezo wangeshaichoma moto.

....mkuu wala hujakosea,.. wametuletea KIGUNDU tena sana maana tumeona haina jinsi ngoja tuwasikilizie katika toleo lingine watakalotangaza japo sisi wanyonge tuliokuwa tumepita KIHALALI kwa imani ya KAMA IPO, Ipo Tu.., Sasa wanaona bora TUKOSE wote mpaka hao waliokuwa WAMEWAPENYEZA kupoza MACHUNGU yao ili NAFASI wawape hao JKT...
 
...HILI SUALA bora lifike Kwa WAZIRI MKUU... Vijana Tunabangaiza, Elimu Tunazo bado TUNABANIWA kwa visingizio vya ajabu kabisaaa...
 
Katibu mkuu kama taarifa hizi ni za kweli bado nitazidi kuulaumu uamuzi wa wizara hii uliochukuliwa..TUTASEMA HATA KAMA WATAZIBA MASIKIO...kitendo cha kuamua kufuta ajira hizi pasipo kuainisha ni akina nani walikuwa na sifa na wangapi hawakuwa na sifa ni dhahiri kwamba bado sio kujisafisha..Hivi ni kweli kuwa wote 228 walipendelewa.wadogo zetu tuliamini kuwa walipita kwa haki ila wengine waliharibu mchakato..Then katibu mkuu amejikingia kifua khs nafsi za mkaguzi msaidizi ambazo zilikuwa na utata sana.kawatoa kafara uhamiaji kajiacha yeye alieongoza kuita maelfu ya watu kwa nafasi 70..amekuwa mwepesi sana kuchukua maamuzi kwa uhamiaji huku alijisafisha upande wake eti hakukua na tatizo...IPO WAPI HAKI YA WALE WALIOFAULU USAILI...HIVI UKISEMA MTIHANI ULIKUWA NA UDANGANYIFU NI KWELI SHULE ZOTE AU WANAFUNZI WOTE WALICHEAT..KILICHOTOKEA UHAMIAJI NI USALITI WA NDANI WATOTO WA WAKUBWA WENGINE WALIACHWA NA IKASABABISHA MTAFARUKU..LAKINI SIO KWAMBA MAMBO YA UNDUGU YATAISHA HADI HII DUNIA ITAKWISHA HATUWEZI KUPINGA NEPOTISM..YANI SIKU HIZI KUJUANA NI SIFA YA ZIADA....KATIBU MKUU RUDISHA WATOTO WA WAKULIMA WALIOFAULU HUKO JKT BADO KUNA NDUGU TU YANI HAKUNA JIPYA
 
Katibu mkuu rudisha watoto wa wakulima na wote waliokuwa na sifa..tuambie nani alikuwa na sifa na nani hakuwa na sifa...bila hivyo hakuna kitalachoendelea hapo..kwani huko jkt kuna wanyama au ni watu walewale...tunajua nepotism ni kansa ila hakuna haki iliyotendeka kwa wengine..watu 228 wote walipendelewa...hii haingii akilini hata kidogo..katibu mkuu uamuzi uliochukua ni dhahiri kuwa uliofanya nao kikao ni mabingwa wa kupora haki.
 
....ngoja niweke mambo sawa NIZAMIE zangu UGHAIBUNI,.. Whatever Litakalonitokea maybe ndo' itakuwa mwisho wa lyf langu.... Yaani kukaa hapa Tz nitapata STRESS tu za bure, kufuzu nilifuzu bila nguvu ya yeyote anayenijua hapo UHAMIAJI halafu watu wachache hata jopo la watu HAMSINI angalau kulichanganua suala hili, mkaamua kutufuta pamoja na wasaliti wenu mliokuwa mmewaweka... AHSANTENI UHAMIAJI.
 
Chanzo cha ndani kabisa kutoka wizarani ya mambo ya ndani !! Nafasi zitatangazwa tena kuanzia wiki ijayo !! Hayo maelezo yaliyotolewa na mleta thread ni mapendekezo ya kamati ya uchunguzi na si lazima yafuatwe!! Mchakato utasimamiwa na wizara husika !!
 
Mh!!! Hii hatare sasa tulisoma ili iweje, tukianzisha biashara TRA daily wako matakoni, ukiwa machinga mitaa ya kariakoo, mgambo ndo hawa... Yani hii nchi haina jema...
 
....wee mkuu #Mgonjwa , bora hii taarifa umeileta muda muafaka,.. Binafsi pia ni MUHANGA kwa waliofutiwa,... Sasa baada ya kusikia post zitapelekwa JKT nikawa nazidi kuumia tu ROHONI..
 
Mi pia ni muhanga wa hii ishu dats y naifatilia kwa karibu sana !! Kesho cheki na gazeti la habari leo ilitakiwa tangu jana ziwe hewani !!! Embu ni pm ct scan mchina fone number yako
 
Mh!!! Hii hatare sasa tulisoma ili iweje, tukianzisha biashara TRA daily wako matakoni, ukiwa machinga mitaa ya kariakoo, mgambo ndo hawa... Yani hii nchi haina jema...

....HUJAKOSEA mkuu.. Hii NCHI unasoma ili UBURUZWE na watawala na WAKUAMULIE watakalo wao...
Example; upuuzi unaoendelea UHAMIAJI... Oveerr!
 
So mpango ni jkt, huko nako urasimu haufai, kwenda tu jkt ni issue
 
Mi pia ni muhanga wa hii ishu dats y naifatilia kwa karibu sana !! Kesho cheki na gazeti la habari leo ilitakiwa tangu jana ziwe hewani !!! Embu ni pm ct scan mchina fone number yako

....haina noma mkuu,.. Ngoja nisikilizie hayo magazeti ya KESHO...
 
Katibu mkuu rudisha watoto wa wakulima na wote waliokuwa na sifa..tuambie nani alikuwa na sifa na nani hakuwa na sifa...bila hivyo hakuna kitalachoendelea hapo..kwani huko jkt kuna wanyama au ni watu walewale...tunajua nepotism ni kansa ila hakuna haki iliyotendeka kwa wengine..watu 228 wote walipendelewa...hii haingii akilini hata kidogo..katibu mkuu uamuzi uliochukua ni dhahiri kuwa uliofanya nao kikao ni mabingwa wa kupora haki.

....sauti zetu ambao tulikuwa tumebahatika kupita KIHALALI zimeminywa... Ngoja tuendelee kuranda randa na Barua za kuomba kazi sehemu zingine..
 
Back
Top Bottom