Ajira za Ualimu sasa ni wimbo,zinatoka kesho usiku

Daaaaa walim punguzen jazba bas kidgo, au ndo ile pressure ya kutaka kupractice kidigital yote mliyojifunza ktk lesson plan na schem of wrk into reality !
 
Bwana awe nanyi katika kipindi
hiki kigumu machopitia! Kuna
usemi nasema Kosa Hela Ujue
Kipaji Chako Na Pata Hela
Ushangae Tamaa Yako! Sasa
katika kipindi hiki msichokuwa na kazi ndo mda wa kujua vipaji
vyenu! Ngoja niwape miongozo
kadhaa jinsi ya kupata kazi
mujini hapa! 1.Recruitment Agencys- Mambo
za kuhangaika na ma CV
imepitwa na wakati, Mambo yote
ni kupeleka CV zenu kwa hawa
agents then wanakuinterview na
kuwalink na Clients wao wa ukweee! ,Mfano RADAR
RECRUITMENT ni agent wa siku
nyingi wa GAPCO na PUMA OIL!
Sasa usitegemee utapata kaz
kubwa kwenye makampuni
makubwa bila hawa magent kupata chao! (Kampuni ndio
inalipa sio wewe) Mimi RADAR
walinipeleka kwa clients 2
tukashindwana maslahi coz mimi
ni mvivu plus nataka pesa nyingi!
Kuna Enrich Africa pia alinipeleka kwa clients 3, wa maana basi tu
mtu ukiwa hujielewi ndo hivo
tena! Kuna EUROLINK
(wanyonyaji sanaaa) Kuna PES
(Wazushi) Shughulika Recruitmen
(Wababaishaji) na wengineo! Jaribuni bahati zenu wadogo
zangu! Kuna mtu alipelekwa
GAPCO na RADAR kwa starting
ya 1.8m enzi hizo ni lawyer huyo
dada.(Let this serve as an
inspiration) 2.Scholarship-Kama GPA zinasoma
poa kuanzia 4 huko kuna
mascholarship ya kumwagaaa
kuanzia Ubalozi wa USA,
JAPAN,CHINA, UK,TURKEY,
RUSSIA na zinginezo! Sasa ushaona hapa na GPA unayo wahi
ubalozi saa 12 sema naulizia
Scholarship nimeambiwa zipo
utaambiwa urudi mwezi wa
ngapi! Na urudi! Sema siwafichi
Mitihani ni Deadly kinomaaa! Mi wa USA ulinitoa knock out lasivo
box zilinihusu sanaaa! Hizi
scholarship za maana atii sio za
wasiwasi kila kitu paid! Sema ndo
ujikamue ufaulu huo mtihani
wao! Baloz zote nilizotaja ndo miezi ya kufuatilia hii, wa 8 ni
kukwea pipa! Sasa kaeni mkingaa
sharubu mujini hapa muione
habari yenu! Na mkienda mbane
huko huko mpate uraia sio
kujifanya vimbelembele front kurudi huku wakati mnaoa hali si
shwari! 3.Mjiunge na Vyama vya Siasa!
Mimi ni CCM damu, na asikwambie
mtu kupata kazi mashirika ya
uma Chama kinahusika sanaaa!
Mnaweza hata kujiunga na chama
cha hao wavaa magwanda ila mtapata network na exposure
kuliko kushinda mnaangalia
Woman of Steel na degree zenu!
CCM is a Plus coz ukiweza kumake
a difference na kujulikana
ushatoka! Kuna watu walijiunga na chama vyuoni now ni
wabunge hawaangaiki na
kudondosha CV 4.Pelekeni CV hizi new banks
zinaajiri japo mboga ndogoo,
ndogo kweli kweli! FMBE, EQUITY,
FNB, NIC BANK, BOA, KCB,FINCA,
AKIBA, BANK M, UBA etc Peleka
zote hizo hutokosa hata moja ila ndo mjue kazi tembo mshahara
sisimizi! Na shurba ya bank isikie
tu kwa wenzio! Highest hapo ni
UBA anatoa starting gross ya
900,000 hadi 2011 saivi siwezi jua
sanaaa! Si haba kuliko kukaa home! 5.Hakuna kazi nzuri ni wewe
mwenyewe tu unavochakarika
kuzispot mishe mishe za ukweee!
Hata kama mishe zinapigwa
wewe hujastukia hupati kitu
kabisaaa! Muwe wajanja wa kucheza na Over Time, kusaka
marupu rupu na kukwapua
inapobidi! Asikwambie mtu hela
ya mishe tamuuu! Ila mkumbuke
za mwizi arobaini! Mkishikwa mie
simoo! Mazingira ya kazi! Nikiwa graduate wa 2010
nishaajiriwa zaidi ya 4 times
sehemu tofauti tofauti! Kazi hizi
za kuajiriwa hazitofautiani ni yale
yale tu! Kampuni jina kubwa
maslah hakunaa! Kila ukihama ni yale yale tu! So kama umeajiriwa
usijione huna bahati ndo hali
halisi, piga mzigo hapo! Watu
wanadanganya mishahara yao!
Ukweli kila mtu anaujua moyoni!
Mtu yuko Auditing Firm jina kubwaa na CPA yake, hiyo Take
home sasa Majanga Majanga!
Akisafiri analipiwa Full Board
baba zimaaa! Ila its better than
nothing! La msingi wadogo zangu
mjipange mjiajiri, mfungue
maconsultacy hata kuleta mizigo
china poa tuu ndo mtatoka ila
huku white collar bado sanaaa!
Sikia tu mwenzio yuko CRDB jina kubwaa uliza Take home!
Majanga plus plus! Tunashia Kuwa
Kopa kopa UNTD tu! Mkopo juu ya
mkopo! Ila kuna watu na bahati zao
wamewin bwana kwenye NGOs
huko, Research, Projects na
waliokaa kwenye Mirija aka
vitengo madhubuti! You never
know na nyie mnaweza kuwa kati ya hao wachache wenye
bahati! Zidisheni maombi!
Otherwise niwatakie Saga Lami
njema!
 
Back
Top Bottom