Ajira za muda zenye kutweza

Ajira za muda zenye kutweza

DREZ

New Member
Joined
Nov 30, 2013
Posts
1
Reaction score
0
Katika pitapita yangu nimegundua kuwa kuna makampuni yana majina makubwa sana na heshima mitaani na midomoni mwa watu. Lakini nilichokibaini ni kwamba kampuni hizi nyingi zinapata faida baada ya kuwanyonya sana vijana, hasa wale wanaohitimu na wasio na ajira.
Mimi nazifananisha kampuni hizi na zile za kikoloni kama British East Africa Company, Germany East Africa Company nk.
Hebu tafakari, unapata kazi ya muda, Eti research, kufanya madodoso, unapelekwa mikoani kwa shilingi 17,000 tu kwa siku, nayo ikukimu malazi, chakula, mawasiliano yako, vinyaji, nk.
Halafu wanakuambia ukirudi baada ya research utapewa sh 10,000 kwa siku ulizofanya kazi, nayo ni baada ya kukagua kazi yote na isiwe na makosa.
Lakini kali zaidi ni kuwa hela hiyo huipati kwa wakati. Kuna taarifa kuwa kuna watu walifanya kazi kama hizo mwaka huu mwezi wa sita na hawajalipwa mpaka leo desemba.
WanaJF hapa ipoje.
 
Kampuni gani hilo? Wafumbue macho vijana wengi pia watakaotoa ushaul wapate pa kuanzia

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
It will be usefull if you name the company/organization here
 
Inategemea ni research gani! sio kila kitu ni kunyonywa mkuu! mbaya nikutolipwa haki yao kwa wakati!
 
Inategemea ni research gani! sio kila kitu ni kunyonywa mkuu! mbaya nikutolipwa haki yao kwa wakati!

Well said.

Tsh. 17,000X30Days=510,000Tsh per month. Not bad.
 
Synovate hao hta mm kna kipindi nilishindwana nao elfu kumi na saba mkoan hujui unalala wp,unakula nn asubuh mpka jioni,mawasiliano na ikumbukwe kwny research kna makundi mengne ili uwafanyie research lazma uwapoze kitu kidgo sasa kwa hela hyo inatosha?

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
hyo kampun kama co nielsen watakuwa synovate hyo ndio michezo yao. Tena nielsen wanalipa 2200 per quationaire. naunatakiwa ucfanye quationaire more than four per day...Huu ni unyonyaji jaman
 
Back
Top Bottom