Ajira-wizara ya kilimo, chakula na ushirika - nafasi 574 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajira-wizara ya kilimo, chakula na ushirika - nafasi 574

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Kubingwa, Nov 10, 2011.

 1. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  WIZARA ya Kilimo, Chakula na Ushirika imetangaza nafasi 574 za kazi katika fani mbalimbali zinazohusu sekta ya kilimo na idara zake.

  Nafasi hizo zinawalenga watu wenye sifa mbalimbali ikiwemo kuwa na umri usiozidi miaka 45 na elimu ya kuanzia Shahada moja na kuendelea kulingana na aina ya kazi.

  Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwa vyombo vya habari juzi na Ofisi ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, waombaji wenye sifa wanapaswa kupeleka barua za maombi katika ofisi yake na wawe tayari kupangiwa kazi wizarani na ofisi za mikoani za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

  Eneo lenye nafasi nyingi za ajira ni Ofisa Kilimo Daraja la II ambapo ajira 378 zitatolewa kwa waombaji wenye sifa za kuwa na Shahada ya Sayansi Kilimo na Mazingira, nafasi zote zikihitaji wahitimu kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambulika na Serikali.

  Aidha, ajira 70 zitatolewa kwa Ofisa Utafiti Kilimo Daraja la II ambapo waombaji wanapaswa kuwa na Shahada ya Kilimo, Uchumi Kilimo, Uhandisi Kilimo, Sayansi ya Chakula na Teknolojia, Sayansi ya Viumbehai na Maabara, Udongo na Mazao (Agronomy), Mazingira na Mazao ya Bustani na Maua.

  Nafasi nyingine 88 ni katika Uhandisi Kilimo Daraja la II na kwa mujibu wa tangazo hilo, waombaji wawe na shahada ya Uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya kilimo, umwagiliaji, ujenzi, ufundi na mazingira.

  Ajira 38 ni za Mkufunzi Kilimo Daraja la II ambapo waombaji watapangiwa kuwa wakufunzi katika vyuo vya kilimo na mifugo vilivyo chini ya Wizara ya Kilimo na ile ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na wanahitajika watu wenye Shahada katika kilimo kutoa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) au kingine kinachotambulika na Serikali.

  Kwa mujibu wa taarifa ya wizara, waombaji wanapaswa kupeleka barua zao siku 14 kuanzia taarifa ilipotolewa katika vyombo vya habari.


  source: Habari leo 10.11.2011
   
 2. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Haya sasa wana SUA mshindwe wenyewe tu.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,434
  Likes Received: 19,774
  Trophy Points: 280
  Ooo hakuna kazi hizo hapo sass bila kimemo test bahati yako usifuate mkumbo wa kulalamika tu.
  Do something!!!
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mkipata link tuwekeeni basi..iwe specific
   
 5. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  kw heri kaka kilimo kwanja sio
   
 6. a

  anonimuz Senior Member

  #6
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 102
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hapa tu ndio ninapowapendea wabongo. What about going to the "Wizara ya Kilimo" page or, at least, buying a news paper. Take some initiative for God's sake. After all, there's everything u might need kwenye hiyo post ya mshikaji: the post title, qualifications, deadline, age limit, where to send ur application (tafuta postal address on website).
   
 7. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  mbona kuna waliodai hakuna ajira mpya zaidi ya ualimu na udaktari? Ngoja na miye mgavi niendelee kujipa moyo.
   
 8. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  si ujiajiri mkuu,we unategemea hi gvt ya wahuni itakukumbuka ni leo kweli?
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Chuo cha kilimo MATI Kilosa Dili hilo
   
 10. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  lol! We senator,hashindwi m2 hapo kama hakutakuwa na ule mtindo wa MUPE MULUKE,a.k.a vimemo!
   
 11. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ngoja niperuzi website ya wizara fasta, vp kuhusu za human nutrition hakuna?
   
 12. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #12
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  mkuu nimeshajiajiri ila lazima niingie huko ili nijibust
   
 13. Blessingme

  Blessingme JF-Expert Member

  #13
  Nov 11, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 250
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  dah kumbe na wew mgavi kama mimi, ngoja tusubiri bana zetu zipo 400
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,133
  Trophy Points: 280
  Haya sasa watu wa SUA kazi kwenu...
   
 15. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #15
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  we mgavi wa wapi? UDSM au?
   
 16. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #16
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,654
  Trophy Points: 280
  Kumbe na hii ni KILIMO, Mimi nilikuwa najua hii ni JIKONI tu?
   
 17. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #17
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  wizara ya kililmo web yao mbona haifunguki?
   
 18. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #18
  Nov 11, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  P*m**u! Huna akili! We umeona jikoni tu! Akili finyu hii!
   
 19. wa kutambua

  wa kutambua Member

  #19
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakuu na sie wa engineering mkisikia mtushitue jaman
   
 20. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  utaona kama ulivyoona hii.
   
Loading...