Ajira mpya ya ualimu: ushauri.

Malolella

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
366
111
Wana jf naombeni ushauri khsu huyu mdogo wangu. Amemaliza degree ya ualimu pale mlimani mwaka jana na akapata nafasi kufundisha private. Huko take home yake ni laki 6 na elfu 30 (630,000/=). Amepangiwa pia serikalini iringa(v) ambako take home ni laki 3 na 81 (381,000). Je aendelee na private au aende serikalini?
 
Yeye kama yeye kwanza anasemaje?Dokezo,private mishahara ni mizuri ila job security ni ndogo.Private waweza fukuzwa kazi any time t,kuna shule za private wanafunzi wakifail somo,mwalimu anawajibishwa.Serikalini mshahara mdogo,sometimes mazingira ya kazi magumu ila job security iko juu,hufukuzwi kazi kirahisi.Akimbia maramoja Iringa akayasome mazingira ya shule hiyo kama yatamfaa kabla ya kuamua kubaki private au kwenda Serikalini.Ila kwa ajira za sasa hivi,bora upate kidogo for 20yrs kuliko kupata pesa nyingi for 5yrs.Ni mawazo tu.
 
Mkuu Aqua kwanza nashkuru kwa ushauri wako. Ameenda kuangalia mazngira iringa v sio mabaya. Huduma zote zipo ie umeme, usafiri, hospital etc. Shida huyu dogo kalewa cheo alichopewa cha usecond master na wanauamini sana paleshule. Mbali ya hyo salary pia analipwa posho ya usecond. Hata yeye yupo dilema. Kote anaona kuzuri japo nimemwambia aende gvt bt naona hanielewi.
 
Wewe umeplay your party,mwache aamue mwenyewe.Ukimlazimisha unavyotaka,baadaye mambo yakiwa magumu atasema wewe ulimlazimisha,yalikuwa maamuzi yako na siyo yake.Ila hata hiyo private anatakiwa ajue,itasurvive industry ya education kwa muda wote,performance ya shule ikoje kimkoa na kitaifa?Nadhani unajua shule za private hupata wanafunzi wengi zinapoperform vizuri na zinaweza kosa kabisa wanafunzi kama waliopita watafail.Sasa hivi ajira ni tight,wasomi kibao wako street,kwa kipindi hiki tulichonacho mi narecommend serikalini.Kuhusu kipato kuwa kidogo unaweza ukatafuta njia zingine za kujiongezea kipato na mambo yakawa poa tu.Ok thanks
 
Mimi nipo serikalini na nimehitimu mwaka mmoja na mdogo wako. Saa yeyote natemana na huu uwalimu . Utafikiri nipo ndani ya thermos ya kahawa.
 
Daa Marko unanifurahisha vp tena? Zingatia ushauri wa Aqua. Thanks sana aqua.
 
Aende private,aache gvt coz,private wanachotaka ni kufaulishiwa wanafunzi tu.GVT hela ndogo,mwambie aende akafanyekazi kwa bidii.Ila asign mkataba wenye faida kwake.
 
Mimi nipo serikalini na nimehitimu mwaka mmoja na mdogo wako. Saa yeyote natemana na huu uwalimu . Utafikiri nipo ndani ya thermos ya kahawa.
baki bwana, sa nani atafundisha watoto zetu jamani ,
 
Wana jf naombeni ushauri khsu huyu mdogo wangu. Amemaliza degree ya ualimu pale mlimani mwaka jana na akapata nafasi kufundisha private. Huko take home yake ni laki 6 na elfu 30 (630,000/=). Amepangiwa pia serikalini iringa(v) ambako take home ni laki 3 na 81 (381,000). Je aendelee na private au aende serikalini?
haiitaji degree ya uhandisi,medisin au law kutoa jibu kwenye hii mada...cheki hali halis ya life hapa bongo..je unadhani mshahara mdogo au mkubwa ni upi utakua helpful?? mwambie aende zake private mkuu!!
 
Tunaishi leo, hatuishi kesho. Hatuhitaji tuzeeke ili tupate mamilioni, tunahitaji kupata sasa tukiwa vijana ili watoto wetu tuwaandalia maisha mazuri......Napita tu ila mwambie atafakari na achukue hatua!
 
Mpe ushauri huu hapa vinginevyo wanae watakuja wamchape fimbo kwa kuwatia umaskini. Walimu wenyewe huko serikalini wanataka kugoma kisa maslahi kidogo halafu yeye aende kufanya nini?
 
381,000/= v/s 630,000/=,kwa laki tatuna themanin utakuwa unakumbatia umasikin mwambie aende praiveti akakusanye pesa ndugu serikalin ni unyonyaji tu,
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom