Ajira isikufanye kuwa Mtumwa...

Ajira isikufanye kuwa Mtumwa...

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Posts
18,682
Reaction score
45,597
Ukosefu wa ajira ni changamoto ya dunia nzima.Kinachotofautisha kati ya nchi moja hadi nyingine ni ukubwa wa tatizo.Kila binadamu hubanwa na mahitaji ambayo kuyatimiza bila pesa haiwezekani.Pia,kupata fedha bila vyanzo ni ngumu.Chanzo kikuu cha mapato kwa wengi ni kuajiriwa,ama serikalini au taasisi binafsi.

Hali hiyo ndio husababisha watu wengine wawe tayari kufanya chochote ili wapate ajira.Wakiombwa rushwa ya fedha hutoa,wapo ambao hulazimika kutumia miili yao kama zawadi kwa mtoa ajira.

Wasio na fedha wanaahidi mishahara ya miezi kadhaa kulingana na makubaliano.Unakuta mtu kaanza kazi,badala ya hali yake kuwa bora kwa sababu ana kipato cha uhakika,maisha ndio yanazidi kuwa magumu.Kumbe anamfanyia kazi mtu.Na wapo wanaogeuzwa watumwa wa mapenzi pia.

Kila mtoa ajira anapohitaji kutimiza matakwa ya mwili wake,anaagiza tuu.Ndani ya ofisi moja unakuta wapo watu hata watano wenye kuchangia penzi la mtoa ajira kwa sababu wamepewa kazi kwa mtindo wa aina moja.

Kutoa rushwa ili kupata kazi ni matokeo ya juu ya kutojitambua.Unapaswa kuelewa kuwa unapoajiriwa maana yake umefuzu vigezo vya ajira,yaani unaonekana unaweza kutekeleza kazi ambayo umeomba na kutengeneza matokeo,sasa rushwa ya nini?

Zipo hasara ambazo utaandamana nazo ikiwa utaingia kazini kwa kutoa rushwa.Ukizielewa zitakuongoza kukataa rushwa ama kuwa mtumwa.

Unapoajiriwa kwa kutoa rushwa maana yake hiyo kazi umepewa na siyo kwamba umefuzu kutokana na vigezo vyako vya kwenye wasifu wa kitaaluma na uzoefu pamoja na jinsi ulivyojibu maswali ya wasaili.

Uliyempa rushwa anakuweka kwenye daraja la watu ambao amewapa kazi kwa kusaidiwa/kubebwa,kwa hiyo atakushurutisha kikazi kwa namna anavyotaka kwa sababu ya kiburi kuwa bila yeye usingepata kazi.

Unaweza kudhani rushwa uliyompa ni kigezo cha yeye kukuheshimu na kujua thamani yako,Hapo unajidanganya,kwani mlipokuwa mnapeana rushwa kuna mahali popote mliandikishiana au kutiliana saini???

Maoni yangu😛amoja na changamoto hii ya ajira tuliyonayo kwa Taifa,hasa kwetu vijana tusikubali kunyanyasika na kuwa watumwa kwa namna yoyote Ile,.pamoja na ugumu wa maisha na dhiki tunazopitia ni bora kuwa huru masikini kuliko tajiri mtumwa..uhuru wetu ni wathamani mnoo kupitia huo unaweza kufanya jambo lako na ukalisimamia kuliko kunyanyasika na kusimangwa.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu tubariki vijana wa Tanzania..
 
Back
Top Bottom