Ajira isikufanye kuwa Mtumwa...

Tufanye plan B tuu babu,.tulio mitaani na diploma zetu tuko wengi na neema ya kutuajiri wote haipo,.na kama ipo si ya leo wala kesho,.ni mchakato
Kujiajili kwa shughuli yoyote ndo mpango mzima ili mradi usiupoteze utu na dhamani yako. Anza sasa kuchunguza ni changamoto zipi zilizopo eneo lako ili uzifanyie kazi.
Tatizo la mtu ndo kazi ya mwingine.
 
Tufanye plan B tuu babu,.tulio mitaani na diploma zetu tuko wengi na neema ya kutuajiri wote haipo,.na kama ipo si ya leo wala kesho,.ni mchakato
Si unaona ndo nlikuwa namwita dadaako joanah ili aje apate material ikiwezekana ajitose kwenye korosho? Mi ni jiniaz sema tu K Vant zimeharibu mfumo wangu wa kumbukumbu mpaka nashindwa kukumbuka kikokotoo kinahusika na Korosho au bunge lisilo na nguvu
 
Hahahahha babu akili yako unaijua mwenyewe, kumbe kumbukumbuku nazo zishaanza kuyeyuka,.lol
 
Kujiajili kwa shughuli yoyote ndo mpango mzima ili mradi usiupoteze utu na dhamani yako. Anza sasa kuchunguza ni changamoto zipi zilizopo eneo lako ili uzifanyie kazi.
Tatizo la mtu ndo kazi ya mwingine.
Yeah changamoto/matatizo ndani ya jamii ndio fursa zetu wajasiriamali,.lakini je,vijana tuna maono na utayari wa kuyaona hayo??kabla hatujapeleka lawama kwa serikali...uwezo huo tunao kama vijana??
 
Mtoa mada twende taratibu, hivi unaujua Ile msemo wa mtumikie kafiri???

Vijana wa siku hizi wanasema kuna misemo imepitwa na wakati, naweza nkakubali lakini hebu tuvae miwani zenye lens tofauti.

Namjua mtu ambae amesoma na hali ya kwao ilikuwa hohehahe, hakuna ajira, vibarua vya kubeba zege vilimfanya apate TB na kadhalika na kadhalika. Akapata mtu mmoja aliemuonea huruma, akamwambia tunakuingiza jeshini lakini mishahara miwili ya mwanzo sio yako. Akakubali na Leo ni mwanajeshi. Anaisaidia familia yake na yeye mwenyewe yake yanamuendea.

Nakubaliana na wewe kwamba isifikie tukawa watumwa, lakini amini amini nakwambieni hali ni mbaya zaidi ya tunavyoiona. Humuhumu jukwaani wapo ambao wamepata ajira zao kwa njia ambazo wanazijua wenyewe na nyengine ni as rushwa mbaya kabisa ya ngono. Na ajira hizo hizo ndio zikawa ukombozi wao na familia zao.
 
Back
Top Bottom