Mother Confessor
JF-Expert Member
- Jan 7, 2016
- 18,596
- 45,225
- Thread starter
- #41
Mtoa mada twende taratibu, hivi unaujua Ile msemo wa mtumikie kafiri???
Vijana wa siku hizi wanasema kuna misemo imepitwa na wakati, naweza nkakubali lakini hebu tuvae miwani zenye lens tofauti.
Namjua mtu ambae amesoma na hali ya kwao ilikuwa hohehahe, hakuna ajira, vibarua vya kubeba zege vilimfanya apate TB na kadhalika na kadhalika. Akapata mtu mmoja aliemuonea huruma, akamwambia tunakuingiza jeshini lakini mishahara miwili ya mwanzo sio yako. Akakubali na Leo ni mwanajeshi. Anaisaidia familia yake na yeye mwenyewe yake yanamuendea.
Nakubaliana na wewe kwamba isifikie tukawa watumwa, lakini amini amini nakwambieni hali ni mbaya zaidi ya tunavyoiona. Humuhumu jukwaani wapo ambao wamepata ajira zao kwa njia ambazo wanazijua wenyewe na nyengine ni as rushwa mbaya kabisa ya ngono. Na ajira hizo hizo ndio zikawa ukombozi wao na familia zao.
Sawa,hilo silibishi na ninaweza kusema hivyo kwa huyo mjeda ni kama bahati,vipi angeambiwa atoe mishahara kwa miezi 6?
Sawa nayo ingepita angekuwa huru(japo mm naww hatujui kama kweli yuko huru au bado ni mtumwa,inawezekana jamaa bado anamtumia akiwa na shida zake binafsi mpaka mtu unakosa raha ya kazi)haya vipi wale ambao wanautumwa endelevu,yeap;wako kazini wana hali nzuri kimaisha watoto wanasoma lakini kuna boss ambaye nyege zikimshika tuu ni unaambiwa akukute chumba namba flan,je huyu kama ni mke/mume wa mtu ndoa yao haiwezi ingia mashakani?
Familia itakuwa na furaha ya kweli?kuna magonjwa,kunyanyasikia nakuumia kisaikolojia n.k..jee kipi bora??maana bado huo ni utumwa pia,.