Ajira 70000 serikali zaanikwa ,zitaanza kutoka mwezi February 2017


PATIGOO

PATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Messages
10,626
Likes
8,996
Points
280
PATIGOO

PATIGOO

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2012
10,626 8,996 280
1481169774558-jpg.443691

Ajira 70,000 serikalini zaanikwa

*Madaktari, wauguzi, walimu wapeta

*Wamo pia wa sekta viwanda, kilimo

BAADA ya kusitisha ajira za umma kwa takribani miezi tisa, Serikali imesema katika mwaka huu wa bajeti itaajiri watu 71,496 kwenye sekta mbalimbali ikiwamo elimu, afya na viwanda.

Hata hivyo, licha ya kutaja idadi ya watumishi wapya wanaotarajiwa kuajiriwa katika mwaka huu wa fedha, Serikali haijaweka bayana ni lini hasa ajira hizo zitaanza kutolewa licha ya kuwa imebaki miezi sita mwaka wa bajeti kumalizika.

Akijibu maswali yaliyoulizwa na Nipashe juu ya lini Serikali itaanza kutoa ajira, baada ya kuzisitisha kwa muda, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Florence Temba, alisema Serikali inatoa fursa za ajira kama ilivyoelezwa katika mpango mwaka wa fedha 2016/17.

Katika majibu hayo aliyoyatoa kwa niaba ya Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, yalibainisha kwamba ajira hizo zitakuwa kwenye sekta ya elimu, afya, kilimo na mifugo.
 
G

GeeM

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2014
Messages
1,901
Likes
1,200
Points
280
G

GeeM

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2014
1,901 1,200 280
Nadhani kwa hali ya kutokuaminiana ilivyo sasa ni bora ikaajiri tu bila kutangaza kwamba inatarajia kuajiri
 
PATIGOO

PATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Messages
10,626
Likes
8,996
Points
280
PATIGOO

PATIGOO

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2012
10,626 8,996 280
Mimi hata siimani hiyo habari mpaka nione zimetolewa.
Mara ngapi wametangaza hivo lakini hakuna lolote.
Ama kweli,,ahad zilikua nying mno bila matendo
 

Forum statistics

Threads 1,274,531
Members 490,721
Posts 30,515,437