Ajinyonga kwa kunyimwa unyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajinyonga kwa kunyimwa unyumba

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mgomba101, Oct 7, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  MKAZI wa Mtaa wa Mpanda Hotel, Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, Nzego Vicent (33), amejiua kwa kujinyonga na kamba baada ya mkewe kumnyima tendo la ndoa.Tukio hilo limetokea hapo juzi majira ya saa 7:30 usiku jirani na nyumba waliyokuwa wakiishi wanandoa hao.Mke wa marehemu huyo aitwaye Agnes Nicodemu, alisema siku ya tukio mumewe ambaye alikuwa ametoka kwenye pombe za kienyeji, alifika nyumbani kwake majira ya saa 6:20 usiku na kumtaka ampe tendo la ndoa.Alisema kutokana na shughuli alizokuwa amezifanya mchana, alimwomba mumewe avumilie hadi siku itakayofuata kwa kile alichomweleza kuwa hakuwa tayari kufanya tendo hilo kwa kuwa alikuwa amechoka.Kwa mujibu wa mama huyo, baada ya kumjibu hivyo, mumewe hakuridhika na ndipo alipoanza kumshutumu kuwa huenda ana mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine."Baada ya hapo alianza kunishambulia kwa kunipiga huku akinitolea maneno ya kunitisha kuwa lazima ataniua kwa panga," alisema mama huyo huku akitoka machozi.Agnes baada ya kuona kipigo kimezidi, anasema aliamua kukimbia nje na mumewe nae aliamua kutoka huku akiwa na mashoka mawili, akaelekea kusikojulikana na kuacha nyumba ikiwa wazi."Ilipofika aubuhi, majira ya saa 12:30 asubuhi, majirani walinifuata na kunieleza kuwa mume wangu amejinyonga kwa katani, jirani na nyumba yetu," alisema.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.Wakati mkazi huyo akijinyonga kwa kunyimwa unyumba.
   
 2. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  duh....
   
 3. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,216
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Huyo ni adui ujinga
   
 4. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  ohhhhhhhh..........
   
 5. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,978
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  well problem solved...huko aendako hana shida ya kunyimwa wala kuomba K
   
 6. p

  pazzy Senior Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 194
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kwakisa hiki lzma tukubali ukizidisha sana pombe nihatari kwani utakosa busara yakufanya maamuzi!lkn kama hyo mama naye ndio ulikuwa ni utaratibu wake wakumnyima ushilikiano mume wake basi hafai kwani alifuata nini kwenye ndoa...raha ya ndoa nikupeana ushilikiano na kuweka mipango ya maendeleo!
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Hii kitu hii
   
 8. CORAL

  CORAL JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,471
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Mpumbavu tu huyo mume! Anakuwa mkali kwa mkewe yeye saa 6 usiku alikuwa wapi? Amevuna alichopanda.
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hata akijinyonga ndo kwanza anawaachia wale walokuwa wakimnyemelea mmkewe wafaudu!!
   
 10. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,285
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  inawezekana hajajinyonga mwenyewe inabdi hapo uchunguzi zaidi ufanyike, na huyo mkewe ahojiwe zaidi,
   
 11. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Hata kama umeoa haimaanishi ndio leseni ya kumbaka mke wako..! Lile tendo bado linabakia kuwa ni la ridhaa.. Mwisho wa ciku ufanye na mkeo afurahie.. Sasa huyu katoka kwenye pombe huko anataka.. Kuambiwa mwenzie amechoka ndo kaja juu..! Ubakaji huo..
   
 12. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,672
  Trophy Points: 280
  Ila hili tatizo la kina baba kunyimwa haki ya ndoa linazidi kukua kila kukicha inabidi tuungane wakina baba tuanzishe taasisi za kutetea wanaume kwa sababu wanawake wamepewa nguvu hadi imepitiliza sasa.
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Chonde Chonde Ulevi Ni Nomaaaaaaaaaaaa!!!
   
 14. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Kweli kumnyima mumeo unyuma ni KUMDHALILISHA YEYE NA UKOO WAKE! Wewe umetolewa mahari, ili uende kumpa mwenzio UNYUMBA KILA ATAPOHITAJI, tena ulikubali mbele za watu huku ukitabasamu kuwa Kwenda kumpa u nyumba mumeo hilo jukumu waliweza na walitaka! WHYYYYYYYY KUMNYIMAAAA!!!!! TENA BILA SABABU YA MSINGI!!!!!!!!!. NIMEMUNA NA HICHI KIFO!!!!!! IT WASNT FARE!!!!
   
 15. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  labda niulize yeye hadi saa sita alikuwa wapi tena ya usiku?
   
 16. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kabisa kabisa, kwanza ile kamba kaipatia wapi, wakati mke wake anasema alitoka na shoka mbili, afu police wanatakiwa wamchunguze huyo mwanamke alikimbilia wapi, kuna harufu harufu ya mke wake kuwa kafanya mauwajai hayo au kuna big deal hapo.
   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  unyumba tu kajinyonga, je ugorofa?
   
 18. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,672
  Trophy Points: 280
  Si alikuwa kwenye vikao vya wazee hujui deal nyingi za kina baba zinapatikana bar?
   
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  yaani huwa sikubaliani na hili la dili zinapatikana bar.

  Hawana ofisi? Au matapeli?

   
 20. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Pointi !
   
Loading...