Ajari ya ndege ya yemen

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Naomba wana JF wanisaidie kufahamu, inakuwaje maiti zote za ndege ya yemen air zinapatikana visiwa vya mafia tu na sio sehemu nyingine? au visiwa hivyo vina nguvu za giza? majibu ya kisayansi ni bora zaidi.
 
We Kaitaba vipi ndugu yangu?
Unataka majibu ya Kisayansi wakati unauliza kitu ambayo si cha kisayansi?
We Ulitaka hao marehemu wapatikane wapi ndo uone hakuna ulozi??
Ajali ni ajali ndugu yangu, ondoa imani za kiswahili kwenye hii mambo haya.
 
Kwanini maiti zisipatikane zanzibar, mombasa, yaani zisambae pwani mbali mbali, cha ajabu zote zinapatikana mafya, na muda mfupi uliopita vipande vya ndege navyo vimepatikana mafya, kulikoni mafya?
 
Mafia ni karibu zaidi ya Comoro kuliko Zanzibar na Mombasa na iko kwa sababu ya pepo za Kusi (southern monsoon) ndio maana baadhi maiti na mabaki ya ndege yameonekana Mafia.
 
Hapa nafikiri kuna jibu au mantiki na nafikiri pia kuwa hapa kuna jibu la kisayansi nililokuwa nategemea.
 
Naam, ki-jiografia Mafia ipo kaskazini mwa Comoro.

Jirudishe kwenye mambo ya muelekeo wa pepo pamoja na mgandamizo wa hewa utaona ni lazima miili mingi itaburuzwa (drifted) kuelekea upepo unakoenda. Hivyo basi ni dhahiri miili na mabaki ya ndege kupatikana katika pwani ya kusini mashariki mwa Tanzania napo ni Mafia na Sio Zanzibar wala Mombasa.
 
Back
Top Bottom