Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Mwezi Mei 21 2018, watu watatu walifariki kutokana na ajali ya gari mali ya kituo cha Uwekezaji(TIC) cha Tanzania, huku uchunguzi wa Polisi ukibainisha kwamba chanzo cha ajali kilitokana na mwendo kasi wa gari uliosababishwa na dereva wa gari hilo.
Julai 29 2018, gari la Wizara ya Viwanda na uwekezaji lilipata ajali wakati dereva wa gari hilo akiwakwepa watembea kwa miguu wawili. Watu wawili walifariki huku wengine kadhaa wakipatwa na majeraha.
Agosti 4 2018, Waziri wa Mali asili na Utalii Dk Khamis Kigwangalla, alipata ajali mbaya iliyopelekea kifo cha mtu mmoja ambapo Waziri Kigwangalla alipata majeraha mabaya na gari alilopanda kuharibika vibaya.
Oktoba 21 2018, wafanyakazi watano wa Wizara ya Kilimo walifariki kwa ajali ya gari wakitumia gari la Serikali, huku ikielezwa kwamba chanzo cha ajali ni mwendokasi uliozidi kiwango.
Novemba 3 2018, Watu saba waliokuwa wakisafiri katika gari STL 6250 mali ya CAG wamekufa papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari SU 41173 mali ya NSSF,