Ajali yasababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara kati ya Dar na Morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali yasababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara kati ya Dar na Morogoro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kidoma, Jun 25, 2012.

 1. K

  Kidoma Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tangu saa mbili usiku gari semi trailer kutoka Kongo lililokuwa limepaki baada ya kuishia mafuta, ghafla lilirudi nyuma bila dereva kisha likajikata kona na kuandika saba.

  Hali hiyo imesababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya njia Dar na Moro na gari zote zinazotumia barabara hiyo. Awali dereva hakuwa na mafuta, hata hivyo baada ya mafuta kupatikana, gari lilishindwa kuondoka. Hakuna usafiri kwa abiria wa barabara kwa nchi nzima ukizingatia nchi inaitegema zaidi barabara hiyo kwa usafiri wa ndani na nchi jirani.

  Hakuna msaada japo saa sita hii ndo gari limekuja kujaribu kuondoa container ili libebwe kwenye gari hilo, hata hivyo bado haionyeshi kufanikiwa maana inaonekana mzigo ni mkubwa na inashindwa kuubeba.
   
 2. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,950
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  duh! Poleni wasafiri
   
 3. K

  Kidoma Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tupo katika eneo jirani na maili mbili, kweli hii ni kasi ya kitanzania tunayoihitajia

  yaani, yamkini kila jitahada zinakwama maana baada ya gari la okwamuzi kuchemsha, nalo limeziba njia na cjui nn kinaendelea maana kila unafuatilia rapid intervention zinazochukuliwa na traffic waliofika eneo la tukio, ndipo kichefuchefu kinapopaa zaid
   
 4. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hii inaonyesha kuwepo na umuhimu wa mabarabara makubwa yenye 4 ways au three way.
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sasa mleta mada, Dar na Morogoro ni "around" kilomita 200, ni wapi kwenye tatizo baina ya Dar na Moro?
   
 6. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Watu wamelalamika sana juu ya hii ishu. Sijui JK yuko wapi aokoe jahazi modern taarab. Halafu hapo ukimuita dhaifu atanuna kweli.
   
 7. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Pole sana mkuu, so mpaka sasa hamjui mtatoka saa ngapi hapo mlipo, na mpo sehemu mbaya kana kwamba magari mengine hayawezi kukatisha kwenye pori na kuendelea na safari??
   
 8. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Gari ya safari ya mbali itaishiwaje mafuta? Huu ni uzembe unaoweza kuua watu wasio na makosa. Katika nchi nyingine kuishiwa mafuta barabarani ni kosa na unapigwa faini kubwa tu kwa kuweka uhai wa watumiaji barabara hatarini
   
 9. K

  Kidoma Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  poleni wanajf, nikiwa stuck kwenye ajali hiyo, ghafla laptop niliokuwa naitumia ilizimika poo, nikiwa natuma updates.
  ni kwamba tafrani ilitokea eneo jirani na maili mbili karibu na mizani kama km 4 hivi. waliokuwa jirani walishuhudia foleni zilizoanzia hapo mpaka ubungo kwa upande wa dar na ruvu kwa upande kuelekea moro.
  gar liliondolewa saa 9 usiku na magari yalitembea kwa mwendo wa kawaida baadaya jam hiyo kuanzia saa 12 asubuhi.

  binafsi mm niliyekuwa nasafiri kwenda dom kwa usafiri wa kuunga, nilifika morogoro na abood saa 2:30 asubuhi na dom nilifika saa 8:15 mchana.

  ilikuwa safari ya kuboa maana haraka nilizikuwanazo ziliishia kuchefuka na nilizidiwa na waliolala wakaanza safari alfajiri ya saa 12.
   
 10. K

  Kidoma Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ilikuwa ajabu kubwa na hatari zaidi gari kubwa (volvo) na thamani kubwa tena limebeba madini likaishiwa mafuta, dereva alikuwa hana hata fedha ya kununua mafuta kwa wa2 waliokusudia kumuuzia, abiria aliyekuwemo kwenye gari hilo alitoa mkopo wa elfu 50 kukwamua hali hiyo; awali watu walidhan dereva alipiga kidebe maana inaelezwa aliondoka na kama lita 1500 hivi.

  tajiri mwenyewe amefika eneo la tukio kama saa nane usiku na gari lililofanikiwa kulikokota gari hilo namzigo wake.
   
 11. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa mtazamo wako huo hata matatizo yako na mumeo atahitajika jk aje kuwapatanisha kwa kuwa ndio mkuu wa nchi!
  hilo suala linawahusu askari wa usalama barabarani,ndio jukumu lao kuongoza magari kuyachunguza uzima na ubovu wake na kuashughulika na ajali zote za barabarani,na jinsi ya kurudisha harakati ya barabara ikifunga kwa ajali au foleni ni jukumu lao!
   
Loading...