Ajali yakutisha yatokea Tegeta njiapanda ya wazo

yamepita masaa, hako chanzo cha ajari ulicholeta, picha wala waliokusudia kufa

umenikera sana mkuu............ najua wewe ni mgeni, lakini thamini basi maisha ya wenzako

hahahahahaaa,,,,,,hivi unapowaka moto mwandishi atauzima au kupiga picha ya moto unaowaka iwe kwake au kwa mwenzie
 
Magari mengi ni mabovu ambayo hayana hadhi ya kuwa barabarani. Watu hawazijui sheria za barabarani au wanazifahamu lakini hawataki kuzifuata. Polisi wanachangia kwa kiasi kikubwa maana watu hawaogopi kabisa utakuta mtu hana leseni wala hajaingia darasani kujifunza sheria za barabarani lakini naye ni dreva ukimuuliza huogopi kukamatwa? Nakujibu nitatoa 30 elfu kisha polisi anaangalia pembeni...Nchi yetu inatisha sana kila kitu ni hovyo hovyo!!!! Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.
 
Inasikitisha sana. Makazi yangu yapo Boko lakini mara nyingine huwa napenda kupumzika hapo KKM Pub japo nipate mbili tatu, kwa kweli taarifa hii imenishtua sana. Mungu alitoa, Mungu ametwaa, jina lake libarikiwe, yeye ndiye ajuaye mwanzo wetu na hatma ya maisha yetu.
 
Ajali yaua sita Dar
Watu wapatao sita wanahofiwa kufa katika ajali iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Tegeta Kibaoni baada ya gari aina ya Scania lililokuwa likitokea kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill kupata hitilafu ya breki na kugonga daladala aina ya Isuzu Journey kisha kuangukia watu waliokuwemo kwenye Baa ya KMM.

Source: IPPMEDIA
 
Ajali mbaya ya kutisha,watu kadhaa wanakusudia kufa majeruh wengi,nawaletea picha na chanzo cha ajar hv punde

Mbali na anayejiua kuna namna nyingine kwa binadamu kukusudia kifo? Basi kama na dereva yumo kwenye wakusudiaji ndio chanzo cha ajali!!!!!!
 
nakumbuka wakati jerry muro akiwa anatangaza tbc aliwahi kuonyesha gari moja ya cements ilkitembea usiku pasipokuwa na taa, magari mengi yanayobeba mifuko ya cements ni mabovu ila ajabu mi kuwa traffic hawayachukulii hatua zozote
 
Ingekuwa jioni labda ingenikuta natafuna kongoro pale. Lakini asubuhi hii, mkoloni kanikamata makalio hapa.

pole sana aisee, mwambie mkoloni aangalie tu, maana vidole vyake virefu sana

Jumamosi tuonane basi tunisia rodi aisee, ngoja nimtafute na G-warawara
 
pole sana aisee, mwambie mkoloni aangalie tu, maana vidole vyake virefu sana

Jumamosi tuonane basi tunisia rodi aisee, ngoja nimtafute na G-warawara
Deal signed. Ntakutambulisha mwanachama mpya LOL
 
Hii hapa

205238_362667980462566_1215837875_n.jpg
 
Mkuu,

Kuna lori lililosheheni simeti kutoka kiwanda cha Wazo limefeli breki wakati likishuka kilima kutokea kiwandani. Likaja kuparamia daladala zilizokuwa zinapakia Abiria nia panda pale. Likazoa daladala moja mpaka kwenye Duka la Vifaa vya ujenzi na Bar ya KMM. Mpishi aliyekuwa kwenye jiko la bar amefariki papo hapo, na abiria waliokuwa ndani ya gari wako nyang'anyang'a. Juhudi za uokoaji zinaendelea lakini dalili zinaonyesha kutakuwa na vifo vingi sana. Hivi sasa bado kichwa cha lori bado kiko ndani ya duka la Vifaa vya ujenzi baada ya kuufumua ukuta na kuzama ndani.

Mungu atunusuru na haya Majanga.

Poleni sana wote mliofikwa na janga hili.

Kusema ukweli ile sehemu imekaa vibaya sana na madaladala yanapenda kusimama na kuchukua abiria pale.

Hii si mara ya kwanza kutokea ajali pale, kuna wakati pia Lori lilishindwa kukata kona na kwenda moja kwa moja brake ikawa lile Duka la vifaa vya ujenzi, bahati kipindi kile hakuna madhara zaidi ya duka kuingiliwa na Lori la cement.

WITO: kwa wenye daldala na abiria kuto simama pale ni pabaya sana.

RIP MAREHEMU wote.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom