Ajali ya Waziri Kigwangala: Je, kila mtanzania anahitaji matibabu bila ubaguzi?

Kweli Tanzania tuko nyuma sana kama yunaaminishwa kuwa helikopta haiwezi kubeba wajeruhi wote na kuwapeleka katika matibabu
bora.
Mwandishi wa habari aliyekufa alikuwa anamhudumia huyo waziri.lakini serikali inashindwa hata kumtaja pamoja na hao wengine walioumia.
Kuna Mwana jf hapa anasema ni kupotosha kusema mtu amekufa ina maana yeye hana habari kabisa kama mwandishi kijana mdogo kabisa kafa katika ajali hiyo! Lol! Afruika tuna riho mbaya na umwinyi mwingi.
Mola atusamehe!
 
Katika ajali hiyo ambayo imezungumzwa sana na vyombo vya habari hasa magazeti wale majeruhi wengine wanne pamoja na dereva hatufahamu hali zao na wanatibiwa wapi. Wengine tungependa kufahamu wanaendeleaje!


Kumbuka mwaka 2007 kama sijakosea alipopata ajali Marehemu Salome Mbatia, je ulisikia au kusoma popote juu ya dereva wa lile gari dogo?

Nilichojifunza ni kwamba watumishi wa viongozi hutumiwa kama vyombo, yanapotokea majanga umuhimu wao huishia pale
 


He was unique
 
Nilipokuwa nikifanya kazi kwenye kampuni moja ya kigeni, wote tulikuwa na bima za aina moja


Ndugu yangu bima za hapa nchini na hasa NHIF haipo kwaajili ya watu wa kipato cha chini, ipo kwaajili ya wanene wa huo mfuko.
 
Siyo kweli kwamba Marekani wanalipa Dola 1000 kwa mwezi kama unavyosema! Kama bima ya afya unapata kupitia kazi unaweza kukatwa dola 90 hadi dola 110 kwa kila paycheck hivyo kwa mwezi ni kuanzia dola 180 hadi 220 kwa mwezi hivyo hapo ni kama $2,160 hadi $2,640 kwa mwaka mmoja, kama huna kazi (most unlikely) unaweza kulipa chini sana au usilipe kama huna pato (income)lakini unapewa bima yenye coverage sawa na anayelipia hapo juu ( refer Obama care au Affordable Care Act-ACA) Co-pay unaweza ukalipa au usilipe kutegemeana na aina ya bima kama Aetna, Blue Cross Blue Shield, Anthem nk. Ukifanya kazi part time contribution yako inakuwa kidogo unaweza ukalipa kila check $50 kwa kila check hivyo kwa check mbili kila mwezi utalipa $ 100 lakini unapata huduma sawa na anayelipa zaidi, Unaweza ukalipa co-pay ya dola 10 au 15 kila unapoenda kumuona daktari au usilipe. Nachosema ni kiwango cha huduma ni sawa, hakuna cha anayepata huduma bora zaidi kwa sababu ni waziri au Gavana. Ushauri wangu ni ku-improve huduma zetu za afya ili ziwafikie wananchi wengi zaidi.....Kama Cuba wanaweza kwanini sisi tushindwe? Wananchi wengi wakiwa na bima hata hizo gharama za matibabu zitapungua.
 
Mkuu umeibua hoja nzuri sana!
Kuhusu bima ya afya mfano NHIF hawagharamii vipimo vyote na sio dawa zote wanagharimia, sembuse ndege! Labda ujiunge na AAR kama una uwezo!
Kuhusu hospitali zetu ndio hivyo tena, vitu vya kuunga-unga havieleweki, maadam wakuu wote wanakaa Dar es Salaam muhimbili ndio inatupiwa jicho zaidi! na sasa hivi wanatupia jicho Ben-Mkapa Dodoma kwa sababu wengi watahamia huko!
Hii ndiyo Tanzania yetu, wananchi wa kawaida tupambane na hali zetu!
 
Mkuu Paschal, hata NHIF kuna vipimo na dawa ambazo hawagharamii!
 
Ndugu yangu bima za hapa nchini na hasa NHIF haipo kwaajili ya watu wa kipato cha chini, ipo kwaajili ya wanene wa huo mfuko.
NHIF inasevu wafanyakazi (3% wewe, 3% mwajiri wako), kuna family package (Nadhani laki saba hivi kwa mwaka), kuna bima toto (50,000 kwa mtoto mmoja kwa mwaka), pia kuna bima mkiwa na kikundi maalum kilichosajiliwa ambapo kila mwanachama anapewa kadi yake! Kwa hiyo usipotoshe sana mkuu!
 
Mkuu Paschal, hata NHIF kuna vipimo na dawa ambazo hawagharamii!
Yes sio tuu kuwa kuna vipimo na dawa hawagharimii, bali kuna magonjwa pia hawatibu na kuna mengine yanahitaji kibali maalum ndipo utibiwe. Lengo sio kufanya ubaguzi, bali kuratibu na kulinganisha na uwezo wa mfuko vinginevyo ukitibu kila kitu, mfuko utafilisika!, mfano mimi hapa nilipo nina complex implant ya neuro stimulus implant, inatumiwa na watu waliopata tatizo linaitwa brachial plexus injury, inauzwa US $ 20,000, inawekewa South Africa, India na Ulaya ba Amerika. Wakitoke Watanzania 100 wanahitaji at a time, mfuko utakuwa na hali gani?. Ndio maana kuna bima za afya na bima za afya, ziko huduma kibao NHIF hawatoi kakini mashirika mengine wanatoa, ikiwemo flying doctors.

Hata hivyo huduma kama hizi, NHIF wanatoa ila kwa kibali maalum
  • Cancer chemotherapy for cancer patients
  • Immunosuppressant medicines for patients, who have organ transplants,
  • Haemodialysis and erythropoietin for patients with renal failure,
  • Reading glasses and special radiological imaging such as CT scan and MRI
  • Medical and Orthopaedic appliances
  • Complex Implants
  • Advanced Cardiac Services
  • Some selected Medicines
  • PolypropyleneMesh
  • EMG needle
  • Dentures
  • Orthodontic Services
  • Radiotherapy services
P.
 


Wanachokisema na reality kwenye huduma ni kama mashariki na magharibi zilivyo mbali
 
Umesomeka mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…