Ajali ya Treni na Lori kati ya Machinga Complex na Mataa ya Chang'ombe

Ajali ya Treni na Lori kati ya Machinga Complex na Mataa ya Chang'ombe

Mshika kibendera wa treni alilala nini? maana hupaswa kuwa na ratiba za upitaji wa treni ili awahi kufunga geti linalozuia magari kupita pindi treni inapokatisha.
 
Manjagata, machinga complex na taa za chang'ombe zimeunganishwa na Kawawa road lakini Kawawa road ina cross reli kitaalamu tunaita LEVELCROSSING hivyo ukikuta barabara sehemu yoyote imekatisha reli, sehemu hiyo iite levelcrossing, inaweza ikawa Mandela levelcrossing, Buguruni levelcrossing ama Vingunguti levelcrossing nk. Kuhusu kugongana kwa gari na train, kimsingi hakuna kugongana, ila kuna train kugongwa kwasababu train imetungiwa sheria na bunge mwaka 1962 ili kuilinda na sababu kubwa, muhimu na ya msingi ni kuwa train haina mbadala wa njia, njia yake ni ya kudumu (PERMANENT WAY) na sehemu zenye msongamano kama hapa Kawawa levelcrosing ilipotokea hii ajali pana flagmen ambao wanazuia magari yasimame train inapopita lakini pia kuna alama za tahadhari kabla ya kuvuka reli.

Asante sana Mkuu kwa maelezo yaliyoshiba! Sasa huyo jamaa Wa roli hakumwona huyo flag man? Sijui huwa yana haraka za kwenda wapi? Sasa msala anao!!
 
Bado tupo kwenye ujima treni kupita njia moja na gari!lakini taratibu ndio mwendo tutafika tu!
 
Ukiishi Tanzania hasa Dar es Salaam inabidi upunguze matumizi ya 'utaratibu' bali kama alivyosema mkulu unachanganya na zako. Kwa maana hiyo hata aina ya uandishi na mleta mada haupishani sana na dereva wa treni, lori na waliojenga barabara!

attachment.php



Aaaa!! Lori limefumuuu, treni haijachunuka hata rangi!
 
Ninachoona hapa bila kujali nani mwenye kosa ni kuwa treni imehama kwenye njia yake, au sio?
Kwa maana hiyo shughuli ya kuliondoa hapo huenda ikachukua muda mrefu na hapo wazee wa 'mchakato' lazima waangukie kwenye 'kufa kufaana', deal nje nje!


Niliona hiyo ajali..nikitokea mataa ya chang'ombe...ni kweli treni ilihama njia kabisaaa iimegeuka km inataka kwenda karume...na pia kuna vyuma mbalimbali vimezaagaa chini vya hilo tren ni km vimecjomoka..foleni yake sasa...mpk katibu round about ya kigogo
 
Hawa madereva wa train hawajui Defensive driving kabisa.Matatizo yao huwa yana tusababishia madhara....wengine wanafanya makusudi kabisa.Inawezekana lorry lilikuwa linapita kufika karibu na reli traffic wa pale junction ya lindi akasimamisha magari.Angalia picha lori limegongwa nyuma kabisa.
 
naona dereva wa treni alijitahidi kulikwepa lori lakini akachelewa.. 🙂
 
Wakuu,

Kuna ajali kati ya Treni na Lori imetokea kati ya Machinga Complex na Mataa ya Chang'ombe.

Wanaotumia njia hiyo wanashauriwa kutumia njia nyingine!
attachment.php

Ana roho ngumu kuligonga treni ni balaa
 
Mshika kibendera wa treni alilala nini? maana hupaswa kuwa na ratiba za upitaji wa treni ili awahi kufunga geti linalozuia magari kupita pindi treni inapokatisha.
naona mwenzangu mgeni na hilo chinjio.hilo gate hata mbuzi anaweza akapita akidhamila.lakini kumbuka ujeuri wa hawa madereva wetu ambao kaanzia utingo(akinyanyaswa na dereva wake)kisha kununua leseni kwa v/insp.mnyanyasaji vilevile!huyu atakuwa na nidhamu kweli?kuwa drv kwake ni archivement sasa
lazima a get even.hii ni human behavior sayari zote.asante.
 
Hawa madereva wa train hawajui Defensive driving kabisa.Matatizo yao huwa yana tusababishia madhara....wengine wanafanya makusudi kabisa.Inawezekana lorry lilikuwa linapita kufika karibu na reli traffic wa pale junction ya lindi akasimamisha magari.Angalia picha lori limegongwa nyuma kabisa.
Ndugu Masumbuko defensive driving ni pale dereva anapokuwa na namna nyingine ya kufanya; kwa dereva wa treni hana namna yoyote ya kukwepa iwe ni gari au mtu lakini ujue treni haina usukani inakata kuruba (curves) kwa nguvu ya msukumo (centrifugal force) na kwa uwiano mahsusi wa reli zote mbili (high and low rails) ambao hutengeneza kitu kinachoitwa CANT (SUPER ELEVETION) hivyo dereva hana chochote cha kudefend asigongwe, na akifunga breki kwa engine peke yake kama hizo zilizogongwa inamchukua mita zaidi ya sitini kusimama kuanzia pale anapo apply break, kwa treni yenye behewa ni kuanzia mita mia nne, hapo dereva wa treni atafanyaje anapokutana na watu wasiofuata sheria za barabarani
 
Back
Top Bottom