Ajali ya Ntokela ilihuzunisha sana

Ajali ya Ntokela ilihuzunisha sana

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
11,180
Reaction score
22,803
Huyu shangazi mpaka leo huwa anaweweseka akikaa tu anaanza kutokwa na machozi ...miaka imepita toka tukio hililimetokea miaka kadhaa iliyopopita. huyu Shangazi alikuwa amekaa home mida flani hivi ana tafakari ukuu wa Muumbaji na Mzunguko wa Dunia ulivyo unavyoleta Usiku na Mchana n.k. Akakumbuka kuwa inapaswa aandae msosi mchana akaona awaache watoto home aende Shamba kuchimba Viazi awaandalie Msosi wa Mchana.

Kule Mbeya kuna Chakula naambiwa kinaitwa KIFUGHE (MCHANGANYIKO WA VIAZI NA MAHARAGWE UNASAGWA) yule shangazi hakujua maskini. Hakujua. Katoka zake home kaelekea shamba kuchimba viazi mpaka anarudi home mida ya saa saba. Watoto hawapo. Akandaa msosi. Akasubiri subiri watoto warudi toka kwenye michezo yao, maana ilikuwa Jumamosi. Akasubiri sana mpaka saa kumi na moja jioni akaona hapana. Akaamua aanze watafuta. Alitafuta sana maskini watoto hawakuwa wakionekana hapo jirani. inaumiza sana.

Kumbe wale watoto wamechukuana na wenzao wengine wakaona la Gari Mchungaji Mwansasu alikuwa ametokea Ntokela amefunga safari yake kuelekea Tukuyu wakaomba Lift maana aliwaona wamesimama wanasubiri usafiri njia hiyo hiyo ambayo alikuwa anaelekea ili awashushe mbele huko yeye aendelee na safari yake. akawapakiza (watoto wa miaka 13 kushuka chini) 18 wakapanda nyuma.

Huyu alikuwa mmoja ya watu ambao walikuwepo katika tukio hilo la kusikitisha kati Uso wa Dunia. haya mambo huwa kwa kuwa yanatokea kwenye nchi zetu hizi yanakuwa si issue sana . unajua ni kama tumeshazoea sana kufa... yaani tumekufa weeee... mpaka inafikia hatua ukisema wamekufa watu 20 kwa mpigo wala Haishtui.

Akawa anapita kwa majirani akiulizia watoto wa kaka yake, walikuwa wawili, akiwa kwa majirani huko akiulizana mambo ya watoto alifika dada jirani analia mikono kaweka kichwani kumuuliza kulikoni mbona walia na mikono umeshika kichwani. ndo akawapa taarifa gari la Coca Cola limegonga watoto 9 wamekufa na 9 Majeruhi hapo Ntokela.

Yule shangazi miaka yote hakuwa akifahamu kuwa ana kipaji cha riadha mpaka siku hiyo maana ndani ya dka chache sana alikuwa eneo la tukio katika namna mbayo mpaka leo watu wanasema hawajahi mwona mtu akikimbia namna ile maishani mwao. watoto 9 walifariki. watoto 9 walikuwa wamejeruhiwa vibaya sana.

Vijana wa Ntokela walihangaika kuwabeba wale watoto na kuwatafutia usafiri wa haraka wa kuwapeleka hospital. wengine katika hali ya huzuni na hasira walichoma moto lile gari la Coca Cola. ni ajali ambayo iliwaumiza wan Ntokela wengi na kwa miaka mingi huwa hawataki kabisa kuikumbuka. iliwaachia huzuni na kumbukumbu mbaya.Huyu Shangazi mpaka leo anaumia sana akikumbuka kumpoteza mtoto wa kaka yake mmoja na mwingine kubaki na Kilema.

Hili gari la Kampuni ya Soda ya Coca Cola. Hili limetokea Kyela linaelekea Mbeya. Dereva alikuwa ameshajichokea na safari za kila siku na mapumziko kidogo. wengine wakisema alikuwa kidogo ameutwika. lakini ni mengi yanasemwa kuhusiana na jambo hili.Hii ajali kwa mujibu wa msimulizi ilitokea Mbeya pale gari la Kampuni ya Soda ya Coca Cola lilipogonga gari jingine lililokuwa na watoto hao 18. mpaka leo Ajali hiyo imekuwa ikikumbusha wengi machungu.
 
Pole Sana. Nimeusoma Kwa Making lakini Sijaona Ulipogusia Tena Watoto wa Shangazi. Ni kati ya Waliokuwa ama ni Kati ya Waliojeruhiwa na Shangazi aliwaona Tena Wanawe??
 
Kuna. Msanii wa mbeya anajiita awilo wa. Mbeya aliwahi imba wimbo kuhusu hili tukio la kusikitisha
 
Pole Sana. Nimeusoma Kwa Making lakini Sijaona Ulipogusia Tena Watoto wa Shangazi. Ni kati ya Waliokuwa ama ni Kati ya Waliojeruhiwa na Shangazi aliwaona Tena Wanawe??
Angalia tena Bob, utaona.
 
Mkuu pole ukiwa sawa naomba uandike kuhusu ule tukio la watu 20 kufa kwenye mkanyagano wakigombania kukanyaga mafuta
 
Back
Top Bottom