Ajali ya Noah balaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali ya Noah balaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 2, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mabaki ya Toyota Noah yakiwa yamepakizwa kwenye kwenye lori katika Kituo cha Polisi Nyanguge kwa ajili ya kupelekwa makao makuu ya Jeshi hilo Mkoa wa Mwanza.


  Taifa limepatwa na janga kubwa kufuatia ajali mbili tofauti kupukutisha maisha ya wanafunzi wanane huku abiria watano wakipoteza maisha na wengine 11 kujeruhiwa, baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana.
  Wanafunzi waliokufa maji baada ya kusombwa na mafuriko wakati wakijaribu kuvuka mto wilayani Ngorongoro kutokana na mvua kubwa iliyonyesha, wakati ajali ilihusisha basi dogo aina ya Toyota Noah ambayo abiria wake wote wamekufa na basi kubwa wilayani Magu, Mwanza.
  Habari ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Liberatus Barlow, zinadai kwamba ajali hiyo ilitokea jana katika barabara kuu ya Mwanza-Musoma.
  Inadaiwa kwamba ajali hiyo ambayo ilihusisha basi na gari dogo la abiria ilitokea jana majira ya saa 2:45 katika Kijiji cha Bulula Kata ya Nyanguge, Tarafa ya Kahangara.
  “Alikuwemo ndugu yangu katika moja ya magari yaliyogongana,” alisema mkazi wa jijini Mwanza ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
  “Ni kweli kuna ajali imeua, chanzo ni dereva wa gari dogo aina ya Noah kugeuka,” alisema Kamanda Barlow.
  Aliongeza kuwa gari hilo lenye namba za usajili T 716 BMV mali ya Mzamilu lilikuwa likitokea Magu mjini kuelekea jijini Mwanza na kugeuka ghafla kurudi Magu.
  Alifafanua kuwa hali iliyosababisha gari hilo kugongana na basi hilo lenye namba za usajili T655 BDP, mali ya kampuni ya Zakaria Wambura lililokuwa likiendeshwa na Aziz Hassan.
  Alisema ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu watano papo hapo waliokuwa ndani ya Noah, akiwemo dereva wake.
  Barlow alisema abiria 11 waliokuwa katika basi hilo walijeruhiwa 10 kati yao walikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Magu kwa matibabu.
  Alisema mmoja wa majeruhi, Mbarouk Taka (52), Mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam amevunjika mkono wa kulia na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa Bugando na kwamba hali yake ilikuwa mbaya.
  Alisema marehemu wanne wametambuliwa ambao ni Deus John Kengele (42), mkazi wa Kiloleli Wilaya ya Ilelema jijini Mwanza na mfanyabiashara, Peter Lubisha (45).
  Wengine ni Emmanule Kapesa (30) na aliyetambuliwa kwa jina moja la Mwinyi, mkazi wa Igoma Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza. Marehemu mmoja bado hajatambuliwa.

  WANAFUNZI WANANE WAFA, WAWILI WANUSIRIKA

  Katika janga la mafuriko, wanafunzi wanane wa Shule ya Msingi Piyaya Sale katika Kata ya Malambo Wilaya ya Ngorongoro, Mkoa wa Arusha,wamekufa maji na wengine wawili kunusurika.
  Miili ya watoto watano ilipatikana na kuzikwa wakati mitatu haijapatikana.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Jumatatu wiki hii jioni baada ya kunyesha kwa mvua kubwa na kujaza maji katika mto Lusokutane.
  Mulongo alisema watoto hao walifariki dunia wakati walipokuwa wakivuka mto huo.
  Alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngorongoro ilikwenda katika eneo la tukio kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji na wananchi ndipo ikagundulika kuwa kati ya watoto 10, wawili waliokolewa wakiwa hai na wanane kutoonekana.
  Aliwataja watoto ambao miili yao ilipatikana na kuzikwa kuwa ni Nemao Saragi (11), Rapaine Lekima (12), Kiasiaya Kima (12), Olanana Lekima (13) na Lekinyori Lemasa (11).
  Kwa mujibu wa Mulongo, watoto ambao miili yao haijapatikana ni Nanyangusi Ndalau (12), Lekinyori Lemasa (11) na Sileti Kakea (9) na walionusurika ni Njiroine Ning'atu (13) na Mapehu Lekima (9).
  Alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Ngorongoro kwa kushirikiana na viongozi wa kijiji na wananchi wanaendelea kutafuta miili ya watoto ambao hawajapatikana.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, alisema tukio hilo linasikitisha na jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi wataendelea kutafuta miili ya watoto ambao hawajapatikana.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  inasikitisha kwa kweli....rip marehemu wote
   
 3. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Innalillah wainailaih rajiuun.
   
 4. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Duh hii hatari
   
 5. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  balaaa kweli kweli R.I.P :hatari:
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  R.I.P wote.
   
 7. mtekula

  mtekula Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  R.I.P Marehemu wote
   
 8. MANI

  MANI Platinum Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Hivi hatuna standards za magari ya abiria au kila gari maadamu lina matairi linaweza kuwa gari la abiria?
   
 9. ngosha2011

  ngosha2011 JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 697
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  hyo ajali niliishuhudia,mungu awalaze marehemu wote mahali pema peponi
   
 10. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Lets thinks loudly!! Such a Mad Driver Who qualify him to be a human been driver!! To make an over turn in a high Way!! What is this type of Irresponsible driver?? Oh God Help Us!! All means of Human been control had failed!! SUMATRA!!!
   
 11. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  rip all yaani nilijua ile noah maana nyengine kumbe ajali ya magu mwanza..
   
 12. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  inasikitisha na inauma sana .... hizi gari aina ya noah aka mchomoko zinaua sana watu na madereva wake wengi hawako makini
   
 13. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nadhani suala hapa c aina/standard ya gari,bali tatizo kubwa naliona ni madereva wetu tulionao,umakini wao,kuheshimu kwao sheria za usalama barabarani. Hii psv course inayofanywa NIT na ndo sherti la sasa kupata driving licence class C sijui inawaivisha vp madereva wetu.
   
Loading...