Ajali ya basi usiku huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali ya basi usiku huu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by peri, Sep 11, 2012.

 1. peri

  peri JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  basi la kampuni ya gairo lilotoka dodoma kuelekea dar limepata ajali nyuma kidogo ya mto ruvu baada ya kufeli breki na kugonga basi lingine kisha kutoka nje ya barabara.
  Namshukuru Mwenyezi Mungu hakuna aliyekufa isipokuwa dreva wa basi ndo alojeruhiwa vibaya sehemu za miguuni.
  Mimi mwenyewe nilikuwa ndani ya basi hilo.
  Vyombo vya usalama vinapaswa kulaumiwa kwani mabasi ya kampuni hiyo ni yale yaliyochakaa kutoka kampuni ya shabib na kuianzishiwa kampuni nyingine.
  Huduma za kampuni hiyo ya gairo ni za usumbufu kwani abiria waliotoka tabora kuelekea dar na moja ya basi hilo walihamishiwa ktk basi lingine walipofika dodoma.
  ALHAMDULILAH namshukuru mungu nimesalimika, hali ilishakuwa mbaya.
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Poleni sana mkuu,afadhali kama hakuna aliyekufa
   
 3. Clarity

  Clarity JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 811
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  poleni na Mungu awabariki mmalizie safari salama
   
 4. peri

  peri JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mkuu shida ya usafiri halafu hauwezi kujua gari bovu kwa kuliangalia nje.
   
 5. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Ungewafyatulia binduki yako, POLE MKUU!
   
 6. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee babaangu kwanini 2napanda mabasi mabovi???? Kabla ujapanda basi kagua matairi ya gari na si siti za gari
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Duh! Mungu wetu mwenye mamlaka tunusuru na majanga haya ya barabarani.

  Leo jioni tena huko Mkoani Mara watu 9 wamepoteza maisha.
  MUNGU MWENYE UTUKUFU UTULINDE SISI WAJA WAKO!

  Poleni majeruhi wote!
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  pole sana mkuu kama hakuna aliyekufa sio mbaya..
   
 9. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Pole sana Mkuu, lakini ahsante kwa taarifa, hopefully msaada utapatikana kwa ajili ya dereva ingawa ni usiku.
   
 10. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Pole sana kwa ajari na hongereni kwa kunusurika. Tunashukuru kwa update
   
 11. peri

  peri JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  ni kweli kabisa mkuu, usafiri hasa wa barabarani umegubikwa na ajali nyingi sana, kama sio rehma na neema za mola wetu wengi tutapoteza maisha au viungo ktk hizi ajali.
  Inasikitisha sana.
   
 12. K

  Kolero JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 493
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Pole sana Mkuu na abira wote , nadhani mamlaka inayohusika na usajili wa makampuni ya usafiri lazima nao ulaumiwe, Gairo na hiyo Shabib ni kitu kinachofanya kazi pamoja, Gairo ni sehemu ya kufanyia hayo yote. Nashangaa kumbe sasa ni makampuni mawili tofauti, ajabu sana.
   
 13. Davie S.M

  Davie S.M JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 720
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu Historia yote ya iyo Kampuni unaijua kwamba Ndio Shabiby ameachana nayo hayo Magari kukuu amenunupa Mabasi Mapya ya Kichina.

  Hujatimiza wajibu
  1.Kutopanda/kugomea basi hilo.
  2.Kuto toa taarifa ubovu wa Basi hilo kwa vyombo husika
  Kwa usalama wenu abiria.

  Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Pole sana perri.
   
 15. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #15
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Jamani poleni sana,na hapo mlipakiwa basi lingine mpaka Dar au mmejitegemea tena. MUNGU awalinde na awaponye wote walioumia
   
 16. peri

  peri JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  nashukuru sana wakuu, mabasi mengine yalokuwa yanatoka mkoani yametuchukua na nimeshafika dar.
   
 17. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  .....poleni kwa ajari: tumshukuru Mungu wote kwa pamoja kwa kuwanusulu.
   
 18. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Poleni sana mkuu. Mabasi mengi ni mabovu sana, leo tumekuta basi la Shambalai lililokuwa linatoka Mtae kuja Dar limepata ajali katika milima ya Lushoto sababu ya kufeli breki.Ili kuepusha ajali dereva akalilazimisha likagonga ukuta wa mlima na likasimama bila kuleta madhara makubwa sana.Na tulipofika Visiga saa 3.30 usiku tukakuta mabasi mawili ya Tashrif yameharibika moja linakuja Dar na jingine linaenda Tanga na tumeyaacha hapo yote yana abiria. Tunamshukuru Mungu ajali hazikuleta maafa.
   
Loading...