Ajali: Watu 50 wanusurika kifo Mlima Nyoka mkoani Mbeya

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,364
2,000


Watu 50 wamenusurika kifo baada ya basi la Mbukio Mission waliokuwa wakisafiria kugongana na lori la mafuta katika eneo la Mlima Nyoka,mkoani Mbeya.Ajali hiyo inaelezwa kuwa imetokana na mwendokasi ambapo basi hilo lilimshinda dereva nguvu wakati akitaka kukwepa lori hilo la mafuta na hivyo kujikuta akisababisha ajali,ambapo baada ya ajali baadhi ya vijana ambao hawakufahamika majina yao mara moja walionekana kuziba maandishi ya basi hilo la abiria kusudi waandindishi waliokuwa wakipiga picha wasipige picha jina la basi hilo, bila kujua sababu ya msingi.

Hata hivyo Dereva wa lori lililokuwa na namba za Usajili T3332 Aaga Bw,Godfrey Lymo(33) yeye amejeruhiwa vibaya kufuatia ajali hiyo.

Chanzo:ITV
 

marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,356
2,000
Naona kuna mtu hapo yupo busy anabandika makaratasi ili kuficha jina la basi, hivi zinamtosha kichwani kweli?
 

manking

JF-Expert Member
Feb 8, 2014
1,308
1,195
Duh hatari! ila mleta habari hujasema basi lilikuwa linatoka wapi kwenda wapi,pole kwa wote.
 

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,011
2,000
Basi la Mbukio Missio muda mfupi baada ya kupata ajali ambayo ilisababishwa na Dereva wa Basi hilo, Hapa vijana wakiwa wamechukua magazeti wakificha jina la Basi hilo lisitambulike kwa wale wanaokuja kushuhudia ajali hiyo, Nia na lengo la kufanya hivyo haijafahamika mpaka sasa.


NIONAVYO: Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali, basi lilikuwa katika mwendokasi sana. Sasa huu uhuni wa kuficha jina ni kutaka kutuhadaa wasafiri kwa maksudi kabisa.
 

Nyasirori

JF-Expert Member
May 3, 2009
300
500
Kwa mkoa wa Mbeya yawezekana ni tabia iliyozoeleka. Niliwahi kukuta gari moja limepinsuka barabara iendayo Tunduma, pia wamefanya hivyo
 

Mmea

Member
Dec 3, 2014
34
0
Nachojiuliza hivyo vitendea kazi(gazet na gundi)kavitoa wapi kwa wakati huo:what::what:inamaana vinaandaliwa rasmi kwa matumiz kama hayo:what::what:jibu ni kuwa wanachofanya madereva hawa matokeo yake wanakuwa wanajua!!aaa tanzania
 

kitomondo1

Member
Oct 2, 2014
99
0
Mi nahis akili zao hazina akili kwan mabas yaliyo mengi ukiyatazama kwa rangi tu unajua hili ni bus fulan kila kampuny ya mabas wana rangi zao so kuficha jina si solution ya kutokujua jina la bus hao ni mapunguani tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom