Kuna taarifa kuwa msiba huo umezua kizaazaa huko Songea, ambako watu wanashikana uchawi sasa. Vimetokea vifo vitatu mfululizo katika familia ya marehemu aliyekuwa anasafirishwa Songea kwa mazishi. Inasemekana baada ya kifo hiki cha juzi wazee waliamua kwenda kwa mganga na kubaini kuwa mke wa kaka mkubwa wa marehemu amewawekea 'tego' wanaukoo wa mumewe ili wapukutike. Inaelezwa kuwa alifanya hivyo baada ya mwanae kufariki ghafla hivi karibuni. Mtu wa karibu anasema mama yule aliapa kulipa kisasi akiamini kwamba mwanae ameuawa kishirikina. Ndipo akaenda kwa mganga mmoja wilayani Tunduru alikopewa dawa ya kuwaangamiza aliohisi kuwa ni wabaya wake. Taarifa zaidi zinadai kaburi la mmoja wa ndugu aliyefariki hivi karibuni lilititia siku ile ya ajali, na choo cha nyumbani pia kilididimia. Ni hatari! Mtoa taarifa anasema ataendelea kunijuza kinachoendelea huko msibani.