Ajali Tena: Imeua 8, ni Cosata Njombe

Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,392
2,000
Imetokea Usiku, kati ya Njombe na Songea kuamkia jana 16.12.13 ikihusisha Canter ya kukodi.

Maiti na Majeruhi walipelekwa hospitali ya Njombe na Mbeya.

Ni marafiki na Wanandugu wakazi wa Sogwe, Mbeya.

Tumempoteza jamaa yetu tupo msibani.

mwitu

JF-Expert Member
Jun 22, 2012
856
0
nimeisikia kwenye radio free matukio imetokea kwenye milima ya rukumbulu. Walikuwa wanatoka mbeya wanaenda kuzika peramiho{songea}
 
Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,132
2,000
Poleni wafiwa
mkuu huu msimu wa mavuno ujiweke tayari tu ..na wala aijalishi mpaka upande nasi utashangaa mpwa umepaki rombo view jamaa anakufwata gafla kumbe wanachukua chao mapema kwa mavuno ya 2014 polen wafw
 
waya jr

Member
Dec 10, 2012
66
125
Imetokea Usiku, kati ya Njombe na Songea kuamkia jana 16.12.13 ikihusisha basi la kukodi, Costa.

Maiti na Majeruhi walipelekwa hospitali ya Njombe na Mbeya.

Ni marafiki na Wanandugu wakazi wa Mbeya, waliotoka msibani Songea.

Tumempoteza jamaa yetu tupo msibani.mkuu hii ajali ilitokana na canter ambayo ilikuwa imetoka na maiti mbeya kijiji cha songwe na inasafirisha kupeleka songea,pipe za brake katika canter hivyo kupelekea gari hiyo kukosa brake,kwa sasa kitongoji cha songwe kina misiba takribani mitano,na wote ni watu wangu wa karibu!MUNGU azidi kuwatia nguvu familia,ndugu,jamaa na marafiki ambao wapo katika kipindi kigumu zaidi
 
sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,537
2,000
Poleni sana wafiwa na marehemu wapumzike kwa amani..

Huu mzimu wa ajali hauwezi kupungua kutokana na combined factors ambazo serikali inazijua zote lakini siku zote wanakuja na maamuzi ya zimamoto.. Mpaka hapo watakapoamua kukaa chini na kulizungumza hili kwa kuwahusisha wadau wote na kisha kuyafanyia kazi mapendekezo ambayo yatakuwa yamefikiwa ndo tutaweza kulipatia ufumbuzi jinamizi hili la ajali ambazo zinaondoa uhai wa wananchi wasio na hatia na kuwatia vilema..
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
58,657
2,000
Poleni wafiwa maana naona mmefiwa tena...

Mungu awape afya wale waliojeruhiwa...
 
MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
1,195
Kuna taarifa kuwa msiba huo umezua kizaazaa huko Songea, ambako watu wanashikana uchawi sasa. Vimetokea vifo vitatu mfululizo katika familia ya marehemu aliyekuwa anasafirishwa Songea kwa mazishi. Inasemekana baada ya kifo hiki cha juzi wazee waliamua kwenda kwa mganga na kubaini kuwa mke wa kaka mkubwa wa marehemu amewawekea 'tego' wanaukoo wa mumewe ili wapukutike. Inaelezwa kuwa alifanya hivyo baada ya mwanae kufariki ghafla hivi karibuni. Mtu wa karibu anasema mama yule aliapa kulipa kisasi akiamini kwamba mwanae ameuawa kishirikina. Ndipo akaenda kwa mganga mmoja wilayani Tunduru alikopewa dawa ya kuwaangamiza aliohisi kuwa ni wabaya wake. Taarifa zaidi zinadai kaburi la mmoja wa ndugu aliyefariki hivi karibuni lilititia siku ile ya ajali, na choo cha nyumbani pia kilididimia. Ni hatari! Mtoa taarifa anasema ataendelea kunijuza kinachoendelea huko msibani.
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,707

Haya mambo mabaya sana, poleni wafiwa
 
Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,392
2,000
Hadi umepoteza rafiki yako humo kwenye ajali bado hujui...???? Poleni sana kwa kufiwa.

We Baba V Ningejuaje gari ni Canter, tafrani za Kishirkina Songea, na Kitongoji cha Songwe kimepoteza 5 kama si wadau wa JF kuchangia? Soma walichochangia wenzako ufunguke.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom