Ajali Mikese: Basi la BM la Dar-Morogoro, wawilii wamepoteza maisha

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Kuna ajali ya Basi la BM imetokea usiku wa kuamkia leo maeneo ya Mikese Morogoro. Basi limegongana na gari lingine na kutumbukia kwenye Korongo.

Walio na taarifa kamili au picha tusaidiane katika kuhabarisha hii ajali.

================

Update:

Waliokufa ni wawili na majeruhi 43.

Chanzo ni mwendo kasi. Sababu kuna gari lilikuwa limeharibika limeegeshwa pembeni. Kukawa kuna semi trailer inatoka Moro uelekeo DSM ikawa inalipita hilo gari lililoharibika. Kabla halijamalizika kulipita, BM ikawa imefika hapo ndio ikaingia katikati ya trailer.

Ajali hii ni ya jana tokea saa nne kasoro usiku.
ajali.jpg
IMG-20160123-WA0024.jpg
IMG-20160123-WA0023.jpg
IMG-20160123-WA0022.jpg
IMG-20160123-WA0021.jpg
 
Kuna ajali ya Basi la BM imetokea usiku wa kuamkia leo maeneo ya Mikese Morogoro. Basi limegongana na gari lingine na kutumbukia kwenye Korongo.

Walo na taarifa kamili au picha tusaidiane katika kuhabarisha hii ajali.
Wengi?! Umejuaje wamekufa wengi. Ulikuwa kwenye eneo la ajali au na wewe umesikia hivyo.
 
Niliacha kupanda BM mambo haya haya, linakimbia alafu nlikaa seat ya mwisho sitasahau.
 
nimepata taarifa kutoka kwa mtu fulan,napenda kutoa wito kwa yeyote mwenye picha naomba atupatie hapa!
 
Back
Top Bottom