Ajali mbaya ya treni

Ajali mbaya ya treni

Game Theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2006
Posts
8,546
Reaction score
898
Habari toka dodoma zinasema treni mbili za mizigo zimegongana uso kwa uso asubuhi hii karibu na stesheni ya zuzu nje kidogo nan mji wa dodoma katika reli ya kati.
Kwa mujibu wa mganga mkuu wa mkoa jumla ya majeruhi saba wamefikishwa hospitali kwa matibabu na hadi sasa mmoja ameshalazwa na wengine wanapata vipimo vya x-ray kabla ya kuamuliwa kama walazwe ama waruhusiwe.
Hadi sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika. Treni moja ilikuw inatoka dodoma kuelekea tabora na ingine ilikuwa inatokea tabora kuelekea dodoma.
 
Sasa ni mara ya pili kwa Treni kugongana kwa kipindi kifupi sana!!! Isijekuwa ni wizi wa mafuta kama ilivyokuwa mwanzo.
 
Anyway, tunashukuru kwamba kwa mujibu wa taarifa yako hakuna vifo.
Lakini vilevile angalau ni treni ya mizigo, ingekuwa ya abiria, nadhani stori ingekuwa tofauti sana na hii.
Pole nyingi kwa majeruhi.
 
Ina maana siku hizi hakuna mastation master? Inakuwaje treni kugongana!?
 
Ina maana siku hizi hakuna mastation master? Inakuwaje treni kugongana!?
Unajua WaTz ni wakaidi na wabishi sana ,sasa inapotokea madereva wa garimoshi wanaona vyombo vyao vinaelekeana kwa mwendo wa kasi ,kila mmoja anafanya ari ya kutokusimama akitegemea mwenziwe ampishe japo njia ni moja,na inakuwa si rahisi kusimamisha michuma hiyo ,mara nyingi wanakuwa na ule msemo wa kukoromea...hasimami mtua apaaa...! na matokeo yake ndio hayo.
 
JK unaona hili kwani haya ni madhara ya kubinausisha shirika,kwani baada ya kusoma hili nimemuhadhia jamaa yangu akasema kwa sasa TRL hakuna station master bali huwa simu wanazo treni husika wanawasiliana
 
Ina maana siku hizi hakuna mastation master? Inakuwaje treni kugongana!?

Limbani, wewe uko dunia ipi??? Kuna hata siku moja umewahi kusikia kuwa Watanzania wako serious. Hakuna Management ya maana ndani ya TRL, sasa hao mastesheni master watakuwa supervised na nani????
 
JK unaona hili kwani haya ni madhara ya kubinausisha shirika,kwani baada ya kusoma hili nimemuhadhia jamaa yangu akasema kwa sasa TRL hakuna station master bali huwa simu wanazo treni husika wanawasiliana

Jamani madereva chondechonde msije mkatumaliza,mnaona hata huyu jamaa kiswahili kinamshinda kuandika kutokana na machungu aliyonayo!
 
Back
Top Bottom