Ajali mbaya ya kutisha Iringa asubuhi hii

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Miili ya wafanyakazi wa barabara Iringa ambao walikufa katika ajali hiyo

Ubongo ukiwa umertapakaa eneo la ajali

Mwili wa dereva Taxi ukiwa bado kutolewa
IMG_0563.JPG
IMG_0566.JPG
IMG_0556.JPG

Ajali mbaya imetokea mjini Iringa asubuhi hii na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo huku abiria waliokuwemo katika fuso wakinusurika katika ajali hiyo.

Mashuhuda waliozungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wamedai kuwa Taxi hiyo yenye namba za usajili T620 ANE ilikuwa ikitokea Ndiuka ikiwapeleka wafanyakazi wa barabara katika eneo la Tanangozi am,bako ujenzi wa barabara kuu ya Iringa -Mbeya uinaendelea. Hata hivyo kabla ya kufika katika eneo hilo la kituo0 cha Mafuta cha Eso dereva wa Taxi hiyo ambaye alikuwa akitaka kulipita gari jingine lililokuwa mbele yake alishindwa kulipita gari hilo baada ya kukutana uso kwa uso la Fuso yenye namba za usajili T897 AQS ambalo lilikuwa limeshehena magunia ya mpunga .

Hivyo kutokana na mwendo kasi ambao Fuso hilo lilikuwa likienda nao na mwendo kasi wa Taxi hiyo uwezekano wa kukwepana ulishindikana na hivyo kupelekea fuso hilo kuigonga Taxi hilo na kuipitia kwa juu na kupelekea vifo vya abiria wawili na dereva wa Taxi hiyo papo hapo .

Jitihada za kuzitoa maiti hizo zinaendelea hadi sasa japo eneo la tukio likiwa limetapakaa ubongo wa maiti hizo za ajali na wasamaria wema wakiendelea kufanya kazi hiyo ya kuzitoa maiti bila ya kutumia kinga yeyote na hivyo idadi kubwa ya wasamaria wema hao waqmeonekana wakiwa wametapakaa damu .
 
Ee Mungu shuka mwenyewe utuponye na ajali hizi, ahsante kwa taarifa candid, inahuzunisha sana yaani jamani huyu shetani ashindwe kabisa, ebu watanzania wenzangu tuungane kwa pamoja kukemea roho za ajali, maana tunechoka kusikia kila siku ajali! ajali!
 
Miili ya wafanyakazi wa barabara Iringa ambao walikufa katika ajali hiyo

Ubongo ukiwa umertapakaa eneo la ajali

Mwili wa dereva Taxi ukiwa bado kutolewa
IMG_0563.JPG
IMG_0566.JPG
IMG_0556.JPG

Ajali mbaya imetokea mjini Iringa asubuhi hii na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo huku abiria waliokuwemo katika fuso wakinusurika katika ajali hiyo.

Mashuhuda waliozungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wamedai kuwa Taxi hiyo yenye namba za usajili T620 ANE ilikuwa ikitokea Ndiuka ikiwapeleka wafanyakazi wa barabara katika eneo la Tanangozi am,bako ujenzi wa barabara kuu ya Iringa -Mbeya uinaendelea. Hata hivyo kabla ya kufika katika eneo hilo la kituo0 cha Mafuta cha Eso dereva wa Taxi hiyo ambaye alikuwa akitaka kulipita gari jingine lililokuwa mbele yake alishindwa kulipita gari hilo baada ya kukutana uso kwa uso la Fuso yenye namba za usajili T897 AQS ambalo lilikuwa limeshehena magunia ya mpunga .

Hivyo kutokana na mwendo kasi ambao Fuso hilo lilikuwa likienda nao na mwendo kasi wa Taxi hiyo uwezekano wa kukwepana ulishindikana na hivyo kupelekea fuso hilo kuigonga Taxi hilo na kuipitia kwa juu na kupelekea vifo vya abiria wawili na dereva wa Taxi hiyo papo hapo .

Jitihada za kuzitoa maiti hizo zinaendelea hadi sasa japo eneo la tukio likiwa limetapakaa ubongo wa maiti hizo za ajali na wasamaria wema wakiendelea kufanya kazi hiyo ya kuzitoa maiti bila ya kutumia kinga yeyote na hivyo idadi kubwa ya wasamaria wema hao waqmeonekana wakiwa wametapakaa damu .

nyingine imetokea mwanza eneo la mkolani, gar colora limeingia kwenye uvungu wa semi. ngoja niende polisi mwanza nikachukue picha za gari hilo.

very sory sana
 
inabidi madereva wa magari yote sijui wapewe semina gani

Kama umekaa sana nchi za ughaibuni, ukirudi bongo utaogopa kushika gari barabarani. Kwani hawashiki sheria kabisa, Ukipanda daladala ndo kabisa. Siku hizi wamejitahidi kuthibiti mwendo wa mabasi ya abiaria, kwani wakifika kizuio cha polisi barabarani mapema kabla ya muda unaotakiwa watakuwa na matatizo, hilo limesaidia kupunguza mwendo.
 
ajali ajali,kila siku ajali unatupotezea maisha ya watanzania wenzetu,hivi wewe ajali ni ibilisi gani wewe?mimi naamini ajali sio neno tu bali ni PEPO LA KUTOA MAUTI!MUNGU AWALAZE PEMA MAREHEMU WOTE,AMEN!
 
Du. Tanzania hii. Tuendelee kusema ni kazi ya Mungu.

Kuna siku mwezi mmoja nilipanda daladala kule temeke sikui wapi yanapounganisha ya kwenda Yombo, daladala moja ilivinja kioo cha nyingine sababu ya kuchomekeana kugombea abiria, mwenzake badala ya kuita polisi alifanya kisasi (retaliation) kwa kufuata na kumkwangua mwenzake. Na akatoroka na hapo wameshalipana hakuna wakumchukulia hatua mwenzake. Uendeshaji bongo balaa, nachagua njia za kupita vinginevyo kibabaja chako kitasukumizwa mtaroni.
 
Back
Top Bottom