Ajali mbaya ya bodaboda

Ajali mbaya ya bodaboda

Magita

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2013
Posts
319
Reaction score
144
Ajali mbaya ya pikipiki imetokea sasaivi katika Kijiji cha Mbwewe kilichopo Wilaya ya Bagamoyo, njia ya kwenda Segera, ajali hii imetokea sasaivi yani bodaboda kwa bodaboda zimegongana na kati ya hao madereva mmoja wapo amefariki dunia papohapo ambaye anaitwa Iddi Mikidadi, na dereva mwingine amejeruhiwa sehemu za kichwa yeye yuko mahututi ambaye anaitwa Juma Hamisi yeye ni mkazi wa katika kijiji cha Kimange, na aliyefariki ni mkazi katika Kijiji cha pongwekiona, mwili wa marehemu hadi sasaivi bado polisi wanaendelea na uchunguzi.
 
Zitamaliza watu inabidi kujihadhari nazo.
 
Pole kwa huyo majeruhi. Yaani sipati Picha boda boda kugongana, inamaana walikuwa hawaonani au ni katika kona? RIP kwa aliyefariki.
 
Jamani nini kifanyike. Hizi bodaboda zinamaliza watu na kuwatia vilema vya maisha. Tangu wameondolewa kodi, hali imezidi kuwa mbaya.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Pole kwa huyo majeruhi. Yaani sipati Picha boda boda kugongana, inamaana walikuwa hawaonani au ni katika kona? RIP kwa aliyefariki.

Kweli ukiiwaza inashangaza, japo kwa style ya uendeshaji wa madereva wengi wa bodaboda LOLOTE KUTOKEA HUNA SABABU YA KUSHANGAA
 
Inasikitisha ila bodaboda wengi wao ni wazembe na wasumbufu kiasi cha kulazimisha ajali kama hizi
 
Inasikitisha ila bodaboda wengi wao ni wazembe na wasumbufu kiasi cha kulazimisha ajali kama hizi

Hawana subira hawa jamaa wakati wote wanataka kulazimisha mambo yawe kama watakavyo. Bora wangekuwa wanajimaliza wenyewe lkn uzembe wao unasababisha hadi abiria kupoteza maisha.
 
Wakati waziri wa fedha anasoma bajeti bungeni alisema tumeondoa Road License kwa boda boda na bajaji ili vijana wafanye kazi sasa.
 
Poleni wafiwa inamaana walikuwa na speed kiasi gani hao waendesha bodaboda Mpaka wakavamiana?
 
duh ndio uwekezaji wetu huu
Inna lillahi wa innaillaihy rajiuun
Ndiyo ajira zilizoahidiwa na Chama Twawala katika kampeni kuomba ridhaa yetu watuongoze. Haya ni majanga.
Wafiwa mwenyezi mungu awajaalie subira kwa hili.
 
miaka 20 ijayo Tanzania litakua taifa lisilo na wazee duniani.!!
 
Back
Top Bottom