Landcruiser
JF-Expert Member
- May 27, 2013
- 1,805
- 599
Ajali mbaya ya pikipiki imetokea sasaivi katika Kijiji cha Mbwewe kilichopo Wilaya ya Bagamoyo, njia ya kwenda Segera, ajali hii imetokea sasaivi yani bodaboda kwa bodaboda zimegongana na kati ya hao madereva mmoja wapo amefariki dunia papohapo ambaye anaitwa Iddi Mikidadi, na dereva mwingine amejeruhiwa sehemu za kichwa yeye yuko mahututi ambaye anaitwa Juma Hamisi yeye ni mkazi wa katika kijiji cha Kimange, na aliyefariki ni mkazi katika Kijiji cha pongwekiona, mwili wa marehemu hadi sasaivi bado polisi wanaendelea na uchunguzi.
uchunguzi wa nini..? au alilishwa sumu akachanganyikiwa akagongana na mwenzake.