Ajali mbaya Traffic Light za njia panda ya Jet/Lumo

Ndiho

JF-Expert Member
Feb 23, 2013
2,306
1,531
Kuna ajali mbaya ya basi la abiria Gongo la Mboto-Masaki imetokea kwenye trafic light za njia panda ya Jet / Lumo.

Taarifa za mashuhuda zinasema watu 4 wamepoteza maisha hapo hapo na wengine wengi kujeruhiwa vibaya. Basi limepondeka vibaya kiasi cha roof yote kung'oka na hata viti.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa hii ajali wanasema dereva wa DCM alimkwepa mwendesha baiskeli na spidi iliyokuwepo hiyo gari ndo dereva ikamshinda na kuanguka mara mbili na kuishia kwenye mstimu wa kuogozea taa maeneo ya jeti karibu na airport.

RIP marehemu wote na majeruhi Mungu awaajaalie afya njema

pic1.jpg


pic2.jpg


pic3.jpg
 
Poleni wafiwa poleni majuruhi poleni familia zote zilifikwa na jangwa hili. Tunawaombea majeruhi wapone haraka na mungu awapokee marehemu wote kwenye makao aliyawaandalia. Amen
 
Hope hilo gari ni DCM maana hayana breki ila yana fujo
 
Aisee umeleta taarifa vizuri saana mkuu,.Ubarikiwe.
Hapo tatizo ni mwendo,maana kwa hali gari ilivyo ni kwamba hata speed ya eneo husika driver alizidisha.

Hapo alikuwa ana cheza zaidi ya 100,maana eneo hilo huwezi kwenda kwa speed kubwa namna hiyo.

Na jinsi gari ilivyovurugika aisee jamaa alikuwa bati sana
 
DCM na landrover ya kizamani si gari la kuamini break kabisa
 
Kifo hakikosi sababu. Wapumzike kwa amani ndugu marehemu
 
Dah! Pole iwafikie ndugu zatu waliofariki na majeruhi. Nawaombea waweze kutengamaa.
 
Nimeikuta hii ajali mida ya saa 7 mchana hivi wakati naenda town.... Ninachojiuliza kwanini DCM huwa zinafumuka hivi?
 
Nmeikuta hii ajari mida ya saa 7 mchana hivi wakati naenda town.... Ninachojiuliza kwanini DCM huwa zinafumuka hivi?
mkuu DCM huwa hazichoki anachoka boss.kinachofanyika body likichoka wanavua mabati yote na kuunga unga mengine kwahiyo likipata ajari lazima lifumuke tuu .na mbaya zaidi kuna mengine huwa mabati yake yanaungwa kwa kupiga ribit
 
mkuu DCM huwa hazichoki anachoka boss.kinachofanyika body likichoka wanavua mabati yote na kuunga unga mengine kwahiyo likipata ajari lazima lifumuke tuu .na mbaya zaidi kuna mengine huwa mabati yake yanaungwa kwa kupiga ribit
Aisee hatari maana ile ya matumbi ilifumuka na hii pia imefumuka hatari...
 
Hilo eneo la jet lumo, ni hatari sana. Nakumbuka mwaka kulitokea ajali mbaya sana hapo
 
Back
Top Bottom