Ajali mbaya: Basi la Sumry laua 14 huko Singida!

Ajali mbaya: Basi la Sumry laua 14 huko Singida!

Leomimi

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2013
Posts
2,547
Reaction score
874
Imetokea usiku huu ajali mbaya maeneo ya Ikungi, Singida ikilihusisha basi la Sumry linalosafiri kati ya Kigoma-Dar.

Inasemekana mwendesha baiskeli alikuwa akivuka barabara lori likamgonga ghafla wanakijiji wamejaa kushangaa tukio na askari akipima ajali ndipo likatokea basi la Sumry na kugonga watu kumi na tatu pamoja na askari ni wa 14 mpaka sasa ndio idadi kamili ya waliopoteza maisha.

Mungu awalaze mahali pema Amina.

==========
ZAIDI:
==========
BREAKING NEWS: WATU 14 WAFARIKI KATIKA AJALI MKOANI SINGIDA USIKU HUU WATU 13 akiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida usiku huu.

Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha eneo hilo.

Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida. Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
SHUHUDA:
Mimi ni shuhuda ambaye nilikuwa ndani ya bus la Al Saedy toka Kigoma kuja Dar na gari letu ndilo lilitumika kuipa escort Sumry ili lifike Police maana taa zake za mbele zilikufa.

Ukweli ni kuwa hao wananchi walitaka kufunga barabara baada ya mwenzao kugongwa na hata Sumry alipowapigia horn waligoma kuondoka na kuendelea na zoezi la kupanga mawe. Dereva wa Sumry alijitahidi kuwakwepa lakini akashindwa kutokana na mwendo kasi na pia kulikuwa na gari jingine mbele yake.

Ubishi wa hawa ndugu zetu ndio umepelekea maafa yote.
 
may God rest their soul in eternal peace. amen
 
jamani poleni hilo basi lilikuwa linatokea wapi kwenda wapi pengine kuna ndugu zetu humo
 
Nimesikiliza breaknewz hapa ITV muda si mrefu inasikitisha sana.......dereva amekimbia kujisalimisha kitu0ni.......R.I.P
 
BREAKING NEWS: WATU 14 WAFARIKI KATIKA AJALI MKOANI SINGIDA USIKU HUU WATU 13 akiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida usiku huu.

Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha eneo hilo.

Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida. Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
 
ndaga mi nataka kujua mana kuna rafiki yangu ana safiri toka mwanza leoo kwenda dar
 
Back
Top Bottom