Ajali jamani tena? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali jamani tena?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magulumangu, Jul 30, 2010.

 1. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakuu nimepata habari leo kuna ajali ya basi la Najimunisa limeua lkn sijui ni wangapi na lilikuwa linaenda wa\pi ila barabara ni ya Dar Mza ila yawezakuwa lilikuwa linaenda Bukoba au kahama...mwenye deteili zaidi jamani nijuzeni......Mungu aweke roho za marehemu pema peponi...amina...
   
 2. senator

  senator JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Wanasema limeua zaidi ya watu 19 na majeruhi kibao lilikuwa likitokea dar kwendaa Bukoba..ajali imetokea maeneo ya Bukombe inasemekana ilikuwa ni ushindani wa kuovatake ndo ikasababisha yote hayo.Naona mpaka kuelekea mwisho wa mwaka tutegemee mengi sana ya namna hii.Mungu azilaze roho za marehemu wasio na hati mahali pema peponi
   
 3. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  dah asante mkuu maana jamaa yangu pia amefariki katika ajali hiyo...nimeumia sana maana ni mtu wa karibu sana na mimi anyway alietoa ndiye aliyetwaa na jina lake lihimidiwe...na hiyo lami we acha tu watatumaliza kwa kweli...
   
 4. senator

  senator JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kwanza pole sana kwa msiba wa jamaa yako wa karibu..afu nimepita pale sunday tu ile barabara inafanyiwa ukarabati mkubwa toka kahama mpaka rwanda so ile lami ya zaman inabanduliwa na weka nyingine kiwango zaidi.wanasema Kagema katoa fungu kujazia lile la msaada wa benki ya africa.
   
 5. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2010
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Hivi ni lini serikali itakuwa serious na hii issue, watu wanakufa kila kukicha na hakuna kinachofanyika. Nionavyo mimi hawa madereva wanastahili kupewa adhabu sawa na wauaji wengine, na matajiri inabidi washikishwe adabu maana baadhi yao wanachochea hizi ajali kwa ushindani kati yao. Wanaajiri madereva wahuni na wengi wao leseni wamezipata kupitia mlango wa nyuma. Tufike mahali matajiri wafidie wafiwa na wale repeat offenders wapewe adhabu za vifungo, faini na kama vipi wafutiwe leseni.
   
 6. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 770
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 180
  Nani atawamaliza, Mungu au?
   
 7. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hizi ajali zitaendelea kutumaliza kwa vile serikali yetu haioni umuhimu wa kufanyia kazi sheria za barabarani na kuwachukulia hatua kali wanaotoa leseni feki,madereva wanao vunja sheria,polisi wa barabarani wanao pokea rushwa na kurekebisha barabara zetu mbovu.

  Ajali zinatumaliza kama kuku lakini husikii kitu chochote kutoka kwa viongozi wa nchi yetu wanachukulia jambo la kawaida kwao.


  Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi na atuepushe na ajali zaidi.
   
 8. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ndugu yangu acha madereva na ushindani watatumaliza sana ndo ilikuwa maana yangu...
   
 9. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkuu mie ndo home huko kila nikikamata njia either mza au kahama...si mmoja tu nadhani jamaa zangu waloumia pia watakuwepo wengi tu maana kila siku wanasafiri...tunashukru kwa lami na pia je madereva na matajiri itakuwaje ajali maana zinazidi ongezeka...nilipita huko mwaka jana mwezi wa saba...mza imekuwa waja leo warudi kesho...
   
 10. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 770
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 180
  Mungu ametoa Mungu ametwaa, ulivyotuambia. Sasa madereva kosa lao nini?
   
 11. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,881
  Likes Received: 20,938
  Trophy Points: 280
  BASI LA NAJMUNISA LAPATA AJALI NA KUSABABISHA VIFO KADHAA!!

  [​IMG] Ajali ya Kanegele - Fuso na Super Najimunisa Kahama Mkoani Shinyanga jana kama unavyoona picha mbalimbali zilizochukuliwa eneo la tukio mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo inayodaiwa kusababisha vifo vya watu 18 . Cha ajabu ajali imetokea mita 10 kutoka katika kizuizi cha askari wa maliasili wanaokagua mazao ya maliasili.
  Katika ajali hiyo inasemekana askari aliyekuwa akisindikiza basi hilo alikatwa kicha baada ya fuso kuharibiwa vibaya na basi. hebu Jionee mwenyewe picha zilizopigwa katikaajali eneo la tukio huko Kanegele kama inavyoonekana Sura ya Basi la Super Najimunisa baada ya Ajali.(Picha na Bernard Kinte wa mtandao wa Wanabidii) ​
  [​IMG] Waokoaji wakitafuta maiti ndani ya Fuso. [​IMG]Eneo la ajali-Kwenye kizuizi cha Kanegele. [​IMG]Baadhi ya wananchi walioshuhudia ajali hiyo wakichungulia Maiti zilizopakjiwa ndani ya magari aina ya Toyota Landcruiser hardtop. [​IMG]Askari wa usalama Barabarani katika eneo la ajali

  ANGALIZO:Ajali hii imetokea karibu kabisa na ROAD BLOCK.....how can this happen??Kwenye vizuizi hivi si magari huwa yanapita taratibu sana kwani kuna ukaguzi hapo au mimi sielewi hizo road block ni za nini.
   
 12. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #12
  Aug 1, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakuna wa kuwajibika na hizi ajali?????? Innocent people are dying just like that.....

  Poleni sana wafiwa
   
Loading...