Ajali daraja la Kigamboni: Mtu mmoja agongwa, afa palepale

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,549
22,095
Mtu mmoja kagongwa leo asubuhi maeneo ya darajani kabisa, taarifa za awali zinaonesha mazingira ya ajali inaonekana ni kwamba mtembea kwa mguu huyo alikuwa anavuka tokea upande wa pili wa daraja,(yaani zinakopita gari za kwenda Kigamboni) na alipovuka upande wa pili gari zitokazo Kigamboni pasipo kuangalia, na ghafla akagongwa na kufariki palepale (haifai hata kuweka picha hapa)

TAHADHARI

Watembea kwa miguu ni vyema kuepuka kuvuka vuka hasa maeneo hatari kama haya, na daladala hasipaswi kusimama kuchukua abiria ziwapo eneo hilo la darajani lililozibwa kwa kingo, abiria kwenda upande wa pili ni hatari.

Yakupasa utembee pembezoni upande njia ya watembea kwa miguu tu na si vinginevyo;

UPDATES;
Kwa maelezo zaidi juu ya daraja bonyeza hapa (
Zijue hatari na changamoto za daraja la Kigamboni kabla hujalitumia)
 
Kwakweli tunashuhudia jinsi watembea kwa miguu wasivojali maisha yao kwa kukatiza hovyo hovyo kwenye daraja hilo! kwa kweli hii ni changamoto kubwa sana kwa pale!

nashauri lijengwe daraja kama la Manzese ama sivyo tutashuhudia mengi sana pale darajani! watu hawana discipline ya kuvuka! wanajivukia tu ! eeeh! waTanzania mpaka kuvuka barabara tufundishwe!

Inna liLLAh wa inna Ilaihi Raajiuun!
 
Kosa la marehemu
Kuna mahali pameulizwa kama kosa lilikuwa la nani? Jamani! Nani katuloga Watanzania? Lengo la mtoa post ni kuwatahadharisha wanaotumia lile daraja. Wewe unakuja na hukumu. Wapi na wapi?
 
mwe mwe mwe mwe mwe mwe (Senga's voice) jamani mbona hivyo! Si ajabu alikuwa anawahi kazini ili asitumbuliwe
 
f80f9339c15ac876c7daf2a3fb05dd51.jpg

e11c9044de9a451dd0332375297a5b0f.jpg
 
Kusema ukweli watembea kwa miguu wanavyokatiza hapo darajani nilijuwa tu ajali kama hii zitatokea, njia yenyewe ya darajani inahamasisha kuendesha kweli kweli! RIP ndugu yetu
 
Back
Top Bottom