AJALI: Basi la Kampuni ya New Force lapata ajali ya kugongana na gari ndogo maeneo ya Iyovi

Naona lawama nyingi kwa New Force, ila sidhani kama ni sahihi kwanza kampuni ina magari mengi sana hivyo pia possibilities za changamoto njiani ni nyingi, na pia ana kwenda safari za mbali ajali nyingine kama hii kosa sio la basi ni gari ndogo.
 
upo site yako ya kushoto unaona bus linatiririka kupitia site ambayo sio yake yaani anapita kulia kwake wewe unafanya maamuz ya ghafla ya kumkwepa kwa kuhamia saiti ya kulia kumbe naye wakati huohuo anaamua kurudi kwenye saiti yake(kushoto kwake) kwasabb wote mpo kwenye kasi mnashindwa kuamua nini cha kufanya na kujikuta mnagomgana...
Hahahahaaaaa, sasa hilo basi litapitaje upande wa gari nyingine? Km ndivyo alikua anaovateki huyu wa gari dogo aliwezaje kukwepea kulia ilhali kuna gari inayotaka kupitwa na hilo basi?
Na kwanini hujajiuliza kwann wa gari dogo asingekwepea kwa kuingia porini kwa upande wake?
 
Mshaambiwa dereva wa gari ndogo ndiyo kaifuata new force watu bado wanalilaumu basi la New force,kwa nini msimuulize dereva wa gari ndogo kwa nini kalifuata basi?
 
Mimi huwa nina kamsemo nikiwa kwenye basi kuwa iyovi kuna bangi imefukizwa pale. Mabasi, malori na magari binafsi huwa yanaenda mwendo wa hatari sana pale kwa kuwa hakuna network, tochi wala askari. Hasa mabasi yakishacheleweshwa na tochi Mikumi/Iringa wanasema wanafidia pale. Yani ile milima na kona badala ya madereva kuchukua tahadhari wao wanachukua advantage ya kutokuwepo kwa sheria eneo lile.

Iyovi is a disaster waiting to happen.
 
Kuna tatizo kubwa na hii kampuni kama kweli siyo matambiko. Kila kukicha ajali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom