AJALI: Basi la kampuni ya Jordan lapata ajali na kuua

AJALI: Basi la kampuni ya Jordan lapata ajali na kuua

jembe afrika

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
7,602
Reaction score
3,781
Basi la kampuni ya Jordan limepinduka na kuua watu 8 Kilometa 6 kutoka mji wa Nzega.

Lilikuwa likitokea Mwanza kwenda Moshi.

Nimepita eneo la tukio, mtu mmoja ndio amefariki papo hapo wengine majeruhi

Basi la kampuni ya Jordan lenye namba za usajili T650 AQZ, linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Moshi limepata ajali maeneo ya Kitangiri, Nzega.Mpaka sasa mtu mmoja amepoteza maisha baada ya kulaliwa na basi hilo.

Basi hilo lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Arusha, linaelezwa kuwa lilipinduka baada ya kumshinda dereva katika eneo lenye kona kali.

Mungu tunusuru.

View attachment 243570

View attachment 243571

IMG-20150415-WA0012.jpg IMG-20150415-WA0015.jpg
 
Attachments

  • IMG-20150415-WA0011.jpg
    IMG-20150415-WA0011.jpg
    25.2 KB · Views: 9,493
Sijui tusemeje sasa, hii inatosha jamani!
Je, na matokeo ya design za barabara zinazoendana na viwango vya BRN - matokeo makubwa sasa au ni harakati za wanasiasa wa Kitanzania kuelekea 2015!?
 
Hivi ina maana Tanzania tuache kusafiri kwa mabasi au??? Mungu rehemu roho za waliopoteza maisha katika ajali hii!!!
 
Serikali haikutakiwa kusalimu amri kwa madereva na wenye mabasi krahisi .

Kova kusema "Madereva Hoyeee" Ubungo amekosea sana!.

Hakupaswa kuwafagillia. Eti hakuna tochi tena kwamaderva/ mabasi wala...... Amefanya kisiasa zaidi

Naisikitikia nchi yangu. Hili lawezekana TZ tuu!
 
Hapa dawa ni serikali kupiga marufuku kusafiri kwa mabasi mpaka uchaguzi upite raia wote wasafiri kwa miguu. Naona wamebanwa kwenye albino wamegeukia kwenye mabasi.

inaweza saidia pia
 
Mkuu hilo linaweza kufanywa na serikali shupavu tu!
 
mungu awarehemu sana marehemu wote.
 
Mungu wangu! Itabidi kuwe na utaratibu rasmi wa kuanza na Sala kabla ya Safari. Uwepo utaratibu wa watu kuomba ( Kil mtu kwa imani yak) walau kwa dakika moja kabla safari hazijaanza. Mungu wetu sio kiziwi hata asitusikie. Inatohsa sasa jamani.
 
Hapa dawa ni serikali kupiga marufuku kusafiri kwa mabasi mpaka uchaguzi upite raia wote wasafiri kwa miguu. Naona wamebanwa kwenye albino wamegeukia kwenye mabasi.

Halafu ukawa ichukue nchi? Mumomumo! Mmepiga kelele nyingi kwny albino sasa mbinu imebadilika!
 
Imefika wakati haya mabasi yafungwe ccctv camera ili trafiki wajue madereva wanaoendesha bila kufuata kanuni za usalama barabarani..
 
Mgomo wa abiria kusafiri utasaidia yule aliyeitisha wa madereva aitishe na wa abiria sasa!! au anafurahia hao madereva wanavyoua watu maana yupo kimyaa mashauzi yote yamemuisha!
 
Back
Top Bottom