Ajali: Basi la Ilyana la Songea - Dar, limepata ajali Njombe

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
36,004
40,865
Ndugu wana jamvi

Nimepata habari toka kwa chanzo cha kuaminika kuwa kuna ajali ya bus la Ilyana litokalo Dar kwenda Songea, ajali imetokea karibu na Kijiji cha Yakobi Njombe na majeruhi wamekuwa wakiwahishwa hospital ya Kibena,

Kama kuna mtu ana ndugu aliyesafiri katika bus hilo leo afuatilie kwa karibu ili kujua hali ya nduguye.
16938653_404371319916325_6995750234878646568_n (1).jpg
17022442_404371559916301_8015233978164690647_n.jpg

Nawasilisha

========

Watu watatu wamefariki na 34 wamejeruhiwa akiwemo mwananke mmoja mjazito katika ajali ya basi la kampuni ya ILYANA yenye namba za usajili T 202 DGK inayofanya safari zake kutoka jijini Dar es salaam mpaka mjini songea mkoani Ruvuma.
 
Ndugu wana jamvi

Nimepata habari toka kwa chanzo cha kuaminika kuwa kuna ajali ya bus la Ilyana litokalo Dar kwenda Songea, ajali imetokea karibu na Kijiji cha Yakobi Njombe na majeruhi wamekuwa wakiwahishwa hospital ya Kibena,

Kama kuna mtu ana ndugu aliyesafiri katika bus hilo leo afuatilie kwa karibu ili kujua hali ya nduguye.

More updates to come

Nawasilisha

Kumbe Trafiki Tanzania walisharuhusu Mabasi kusafiri Saa 6 usiku huu hadi kuchwee?
 
Kazi kwelikweli, kwao udhibiti ni mchana usiku wajijue, inatakiwa kama kweli wana nia ya dhati ya kuyazuia wafunge vyombo vya kuya monitor digitally kupitia satellites,

Yaani waache kubanduana usiku huu wakae kusumbuka na sisi Vichwa ngumu?
 
Ajali imetokea mida ya saa mbili usiku. Na sio saa sita kama baadhi ya wadau wanavyosema. Chanzo TBC Taifa; taarifa ya habari ya saa sita usiku.
 
Sasa Ajali kumbe ni ya tokea Saa 2 usiku na tayari hata TBC Taifa walishaifanyia coverage mnavyoileta huku Saa 6 na Nusu za Usiku mnataka tuwaelewe vipi? au mmeambiwa pengine waliosababisha hiyo Ajali wapo humu humu JF?
 
Nami nimepata habari majira hayo nilipotuma, anyway mjumbe hauawi, sikufahamu kama TBC wametangaza maana sina usumaku na TBC, isitoshe JF ina wadau wengi kuliko hiyo stesheni
 
Ajali imetokea mida ya saa mbili usiku. Na sio saa sita kama baadhi ya wadau wanavyosema. Chanzo TBC Taifa; taarifa ya habari ya saa sita usiku.
Ni sahihi maana hizi gari huwa zinafika Njombe saa kumi na mbili jioni,tena kufika saa 2 ilichelewa huenda ilikuwa na shida njiani
 
Kuna taarifa kuwa basi la kampuni ya ilyana limepata ajali na kuuwa maeneo ya njombe usiku wa Jana tar 2 mwezi wa 3. Mwenye taarifa za uthibitisho tafadhari atujuze au kwa wakazi waNjombe tunaomba mtujuze kuhusu hili
 
*HABARI MBAYA.*
Kama una ndugu yako alisafiri siku ya jana Alhamisi tarehe 02/03/2017 kwa *BASI LA ILYANA* Kutoka Dar es salaam kwenda Songea mkoani Ruvuma, Ajaribu kufuatilia huko maeneo kati kibena au Kifanya, Basi hilo limepata ajali na majeruhi wamekimbizwa hospital ya kibena mkoani Njombe.

Hali za majeruhi si nzuri.

Ajali imetokea usiku wa kuamkia leo.

Hii habari nimeipata magroup mbalimbali ya whatsap sijaelewa kama ni kweli au si kwelo,kwa mwenye uhakika tujuze
 
Ni kweli ajali imetokea .... watu 3 wamepoteza maisha na 28 kujeruhiwa kati yao mama mjamzito miezi 7 hali yake si njema
 
Back
Top Bottom