Ajali barabarani yasababisha mtu kuuawa kwa kuchomwa kisu ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali barabarani yasababisha mtu kuuawa kwa kuchomwa kisu !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kilimanjaro, Aug 26, 2008.

 1. K

  Kilimanjaro Member

  #1
  Aug 26, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukusimulia tukio hilo, utadhani ni zile hadithi za kubuni za elfu lela ulela siku alfu na moja. Lakini amini usiamini, limetokea Jijini Dar es Salaam.

  Mtu katoka nyumbani kwake salama, akavuka barabara salama, akapanda basi salama, halafu akauawa akiwa ndani ya daladala!

  Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Kandihabi amesema tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana mishale ya saa 3: 45 usiku katika barabara ya Kilwa eneo la Madafu Jijini.

  Amemtaja aliyeuawa kuwa ni Suleiman Namumila, mkazi wa Mbagala Kwa Mangaya aliyekuwa kwenye daladala yenye nambari za usajili T989 ARL aina ya Toyota DCM inayofanya safari zake kati ya Mwenge na Mbagala.

  Akisimulia mkasa huo kwa undani, Kamanda Kandihabi amesema kwenye daladala hiyo alipanda abiria mmoja mwenye asili ya Kiarabu, ambaye alianza kuzozana na konda akidai amepilizwa kituo.

  Kwa mujibu wa Kamanda Kandihabi, mzozo huo ulianza mara baada ya daladala hiyo kuondoka kituo cha Kwa Aziz Ally ambapo abiria huyo alidai kuwa alipaswa kushushwa.
  Akasema gari hiyo ilipofika kwenye kituo cha Kwa Madafu, ikasimama ili abiria huyo ashuke.

  Hata hivyo akasema wakati abiria huyo akishuka, alimkaba na kumkunja shati konda wa daladala aitwaye Yusuph Hassan, 27, akidai kuwa ndiye aliyesababisha yeye apitilize kituo chake cha kushukia.

  Kamanda Kandihabi akasema baada ya abiria wengine kuona hivyo, wakaingilia kati kumtetea konda wao, kwa madai kuwa abiria huyo amepitiliza kituo chake kutokana na uzembe, kwa kuwa gari lilisimama pale kwa Aziz Ally.

  Akasema Mwarabu huyo alipoona abiria wote wanamjia juu, akachomoa kisu kutoka mfukoni na kumchoma kifuani Suleiman ambaye alionekana kuwa alikuwa akimsaidia konda.

  Akasema baada ya tukio hilo, Suleiman alikimbizwa katika hospitali ya Temeke kwa matibabu, lakini alifariki wakiwa njiani.

  Kamanda Kandihabi amesema Mwarabu huyo baada ya kumchoma kisu Suleiman alikimbia na jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta
  .

  Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Temeke.

  SOURCE: Alasiri
   
  Last edited by a moderator: Aug 26, 2008
 2. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Sio sahihi. Salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu ILA kosa akitenda mtu mmoja haimaanishi watu wote wa asili yake ni wahalifu pia.

  A cheap sensationalist headline, you can do better
   
 3. m

  mkombosi Senior Member

  #3
  Aug 26, 2008
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  alimkaba na kumkunja shati konda wa daladala aitwaye Yusuph Hassan, 27,

  Habari wanaJF

  Nimeipokea habari hii kwa msikitiko makubwa.

  Hawa watu wanapata wapi jeuri ya kumkaba koo Mtu mweusi,mtanzania mwenzetu?

  Wadugu,nchi hii tulipigana kwa hali na mali kuwaondoa wazungu na waarabu,damu zetu(weusi) zilimwagika,hivyo basi tuna kila sababu ya kulinda na kutunza heshima tulioachiwa na wazee wetu.

  Mzee mwanakajiji,plse plse call IGP na mshinikize atupe picha za huyu kiumbe na hatima yake ndani ya mahakama zetu.

  Mpaka kieleweke.
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Na Ditto alikuwa Mwarabu? Acheni hizo!
   
 5. m

  mkombosi Senior Member

  #5
  Aug 26, 2008
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmhhh,kuna kiumbe kipo tayari kutetea mwarabu kuliko mtanzania mwenzake??!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  WaTanganyika,mnaoishi nchi za uarabuni,mnayo jeuri ya kuwakwida makonda wa huko???na mkifanya ivo hatima yake ni nini?

  Tumeingiliwaaaa.....
   
 6. m

  mkombosi Senior Member

  #6
  Aug 26, 2008
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alikuwa babu yako.
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi waswahili hatujawahi kuua waarabu? Na hivi huyo anayeitwa mwarabu ni mwarabu kweli au anaonekana ana damu ya mwarabu? Akamatwe, afungwe lakini si kwa sababu ana damu ya mwarabu.

  Tunakoelekea siko!
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kamanda una walakini...
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Huu uandishi wa KIJINGA ndio unasababisha mjadala wa KIJINGA. Kwani huyo aliyeua aliandikisha mahali akasema yeye ni mwarabu? Kama ni mtu mwenye asili ya Kijerumani na akaonekana mweupe basi ni mwarabu, kama ni mweupe tu naye anaweza kuitwa mwarabu.... lakini pamoja na makosa hayo, jamani suala la kuwa na kauli za kibaguzi ni kosa la jinai. Kwanza mode abadili hata headline ni HATARI.
   
 10. m

  mkombosi Senior Member

  #10
  Aug 26, 2008
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  A cheap sensationalist headline,

  Huna akili timamu wewe,polepole mirembe panakwita.
   
 11. m

  mkombosi Senior Member

  #11
  Aug 26, 2008
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wako ulio bora ni upi sasa?wa kutetea muuaji?

  .

  Unapaswa kubadili tabia yako kwanza ya kutetea waarabu,na uwe mzalendo.

  Akili yako ilivyo mbovu inaona headline kuwa hatari sana,kuliko ya mauaji ya mtanzania mwenzetu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Wewe bwege kweli.
   
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  HAkuna anayetetea mauaji, lakini hakuna anayetetea matusi na ubaguzi wa kijinga. Hata Ditopile alimuua Mtanzania mwenzetu na ndio maana tulimshupalia. Sasa wewe unaleta ubaguzi bila ya kuwa na ushahidi. Nadhani unahitaji USHAURI NASAHA
   
 13. e

  eddy JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2008
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,397
  Likes Received: 3,781
  Trophy Points: 280
  Hizi kauli za kibaguzi naona tusizipe nafasi, huyu nimhalifu tu, bila kujali anarangi gani. Tunajua jf inawapumbavu wehu wendawazimu lakini wenye busara kama FMES na MKJ wapo pia, tunaomba itumike busara katika kuweka post.
   
 14. e

  eddy JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2008
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,397
  Likes Received: 3,781
  Trophy Points: 280
  Halisi, pole sana, unajua hawa mafundi PBX waliosoma univesite computingi senta na maripota waliofeli fom fo wanatusumbua kweli humu, any way mkutano wa hadhara wanahudhuria nawasiohusika.
   
 15. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Naupinga ubaguzi na haswa ubaguzi wa rangi, haiwezekani kujiona kuwa eti uu mzalendo kwa kuwa wewe ni mwenye ngozi nyeusi, wapo wenye ngozi nyeusi ila hawana hata chembe ya uzalendo na wapo wenye ngozi nyeupe ila uzalendo wao hautiliwi mashaka hata kidogo.
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  "bwege", "mirembe inakusubiri", "akili yako mbovu", "Ditto babu yako". Kauli hizi zinatisha kama sio kusikitisha.
   
 17. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  mh! tunajadili mambo kwa uchaga, unyakyusa na sasa uarabu! hakuna takayepona katika ubaguzi huu.

  la maana kuwe na namna ya kuweka utaratibu mzuri kuhakikisha wanaosafiri kwenye vyombo vyetu wawe ni salama. ni vema ikatungwa sheria kuwa ni marufuku mtu kusafir na silaha kwenye public transport

  last time nilisafiri na basi toka njmbe kuja makambako, kuna mtu alipanda na msumeno wa kupasulia mbao, wenye urefu wa mita kama nne, mkali ile mbaya, njia nzima nilisali kusitokee ajali hata ndogo kwa kuwa msumeno ule ambao mwenye nao alisimama kwenye korido ya basi ungetumaliza. nilisali pia kusiwepo ugomvi kwenye basi
   
 18. w

  wajinga Senior Member

  #18
  Aug 26, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  when they came for the jews i did not say anything because i was not a jew,when they came for christians i did not say anything because l was not a christians,when they came for moslems i did not say anything because l was not a moslem,when they came for comunist i did not say anything because l was not a comunist,when they came for th socialists i did not say anything because i was not a socialists .when they came for my neighbours did not say anything because i did not like them anyway.When they came for me there was no one left to speak for me.
   
 19. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #19
  Aug 26, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  shetani tu, tena jini makata linalopenda damudamu, ndo lilikuwa ndani ya huyu mwarabu. roho chafu kama hiyo ingeweza kuwa ndani ya mtu yeyote, awe mzungu, mweusi au mhindi na mwarabu. kuna watu weusi wengi tu wanawaua wenzao kila siku hapa, ukianzia maalbino, kuchunana ngozi,kuua wenye vipara, na mambo mengi sana yanatokea. tunatakiwa kuzilaumu hizo roho chafu ndani yao, sio kuwalaumu wao binafsi kwasababu wao sio wao, hawana nguvu ya kuishinda dhambi kama hiyo(be it black, arab or whoever would be), aliyeshinda dhambi ni Yesu Kristo, na ni kwa njia ya huyo tu tunaweza kuishinda nguvu ya dhambi. hivyo, watu wote, regardless of colour that you are mentioning here, tunatakiwa tumpokee Yesu awe mwokozi wa maisha yetu, msipofanya hivyo, maroho ya shetani yanaweza kuwaongoza kufanya lolote, si ajabu na wewe ukajikuta unafanya hivyo kwa mwingine siku moje because hauna nguvu yoyote kuishinda dhambi. Shetani ana nguvu kuliko wanadamu wote, isipokuwa kwa wale tu waliookoka, hao ndio shetani anawapigia magoti na kuwakimbia. ila wote wasiompokea Yesu, na kumfuata, wako chini ya dhambi/sheria ya dhambi siku zote. msimulaumu huyo mwarabu tafadhali..

  Nasema hivi, kwasababu utakuwa yeye mwenyewe alifanya bila kutegemea, huko aliko anajilaumu sana kwanini amefanya kitu kama hicho. lazima anajilaumu na kulia hadi machozi, kungekuwa na chance ingine, hakika asingeua tena, ila kwasababu imeshatokea, anakosa amani, anakimbiakimbia tu hata raha hana, kama ange anticipate icho kitu, asingekitenda. hiyo ndo inadhihirisha kuwa si yeye, ile roho chafu iliyoko ndani yake ndo ya kuilaumu na kuipiga. yeye ni kiumbe wa Mungu na Mungu bado anampenda pamoja na kwamba ameua. akirudi na kutubu Mungu atamsamehe hata kama ameua. God bless you.
   
 20. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2008
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Baaasii!! pinguzeni munkari jamani...naona mnataka kuchomana visu humu humu JF
   
Loading...