Ajali barabara ya Dar - Lindi, Fuso imegongana na Nissan, dereva kapoteza maisha

Clarity

JF-Expert Member
Jul 6, 2010
1,741
2,488
Nimekuta ajali mbaya ikihusisha magari mawili fuso ikitokea Dar kuelekea Lindi imegongana uso kwa uso na Nissan Serena.

Dereva wa Nissan Serena namba T 755 CLX amefariki papo hapo ajali imetokea muda wa saa 12 :30 asubuhi
18581962_124270434811586_868341047265634528_n.jpg
18486006_124270368144926_1361579782960657885_n.jpg

Ajali imetokea njia ya Lindi kwenda Dar, dereva wa gari ndogo kafariki papo hapo. Pichani hapa ni dereva alie fariki. Tusambaze picha hiii labda ndugu anaweza kupatikana.
 
Nimekuta ajali mbaya ikihusisha magari mawili fuso ikitokea Dar kuelekea Lindi imegongana uso kwa uso na Nissan Serena.

Dereva wa Nissan Serena namba T 755 CLX amefariki papo hapo ajali imetokea muda wa saa 12 :30 asubuhi
Pole kwa wafiwa.
Hiyo njia huwa ni nadra sana kutokea ajali kwakua haipo busy,imetokea maeneo gani?
 
Bora wewe hukujishughulisha kumpiga picha marehemu ili urushe picha hizo mitandaoni. bila shaka ulikuwa bize na uokoaji.
Wafiwa na wahanga poleni sana
 
Weka picha ya hayo magari tuone ila Dereva msitiri mkuu apumzike kwa amani
 
Weka picha ya hayo magari tuone ila Dereva msitiri mkuu apumzike kwa amani
Hata kama asipoweka picha we inakuhusu nini,si ushaambiwa dereva wa gari ndogo kafari au unataka uone maiti ili iweje sasa kwani huamini?
 
Hata kama asipoweka picha we inakuhusu nini,si ushaambiwa dereva wa gari ndogo kafari au unataka uone maiti ili iweje sasa kwani huamini?
Elewa post kwanza..sijasema maiti ioneshwe bali Magari tu....Hivi huwa unasoma na kuelewa au ndio stress za vyeti feki...

Punguza jazba mkuu
 
RIP. Hizo badges zao inabidi ziongezewe na namba za simu za kiongozi wa zone. Inaonekana alikuwa kwenye suicidal speed.
 
Hii barabara ya kusini ni nyembamba na konakona zake duh kipande kipana ni maeneo ya rufiji tu.
 
Elewa post kwanza..sijasema maiti ioneshwe bali Magari tu....Hivi huwa unasoma na kuelewa au ndio stress za vyeti feki...

Punguza jazba mkuu

Naww umewaka mkuu inawezekana na wewe upo kwenye orodha ya vyeti feki
 
Back
Top Bottom