Ajali Arusha: Ndege imetua kwenye Shamba la Mtu

tzbuddy

Member
Mar 12, 2014
33
49
14690860_1082559265175081_4150737594220200107_n (1).jpg

Ndege moja Aina ya Caravan yenye abiria 5 na rubani mmoja,Imelazimika kutua Kwa Dharura kwenye Shamba moja Pembeni Mwa kiwanja cha Arusha . Inasemekana ndege hiyo ilipata engine Failure mara baada ya kupaa.Uchunguzi bado unaendelea kufuatana na Tukio hilo.

Pia pongezi kwa Rubani aliyeweza kuokoa maisha ya abiria Hao na ndege kwa ujumla maana haijaharibika.Wengine wenye latest wataendelea kuchangia.

=====

Watu watano wamenusurika kifo baada ya ndege waliokuwa wanasafiria kutoka katika uwanja mdogo wa Arusha kupata hitilafu kwenye injini yake muda mfupi baada ya kuruka.

Kaimu meneja wa uwanja wa ndege wa Arusha Bw, Bashiru Juma amesema ajali hiyo imetokea saa sita na dakika hamsini na tano ikiwa ni dakika tano tu baada ya kuruka ikiwa na abiria wanne na rubani mmoja ikiwa inatoka kwenye uwanja huo kwenda kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kimanjaro.

Kwa mujibu wa Bw Bashiru ajali hiyo ya ndege aina ya Caravan 5h Zeb ya kampuni ya Coastal Air haikuleta madhara na abiria wote pamoja na rubani wametoka salama na pia hakuna uharibifu wowote unaoonekana kwa macho kwenye ndege hoyo na kwamba taratibu vyombo vinavyohusika na masuala ya anga kuchunguza tukio hilo zinaendelea.

Kwa upande mtendaji wa kampuni ya hiyo ya Caoastal Air nchini Capten Dmond Julian amesema abiria walikuwa wanne wawili raia wa ujerumani na wawili raia wa italia na walikuwa walikuwa wanakwenda Zanzibar.

Chanzo: ITV
 
Unampongeza rubani kwani hiyo ndege ni chopa useme ikitangamaa itatoka hapo? Hiyo ni skrepa tu
 
Ni ndege ya aina gani? Maana juzi pia kuna mtu alianguka na ndege pia
 
Ndege moja Aina ya Caravan yenye abiria 5 na rubani mmoja,Imelazimika kutua Kwa Dharura kwenye Shamba moja Pembeni Mwa kiwanja cha Arusha . Inasemekana ndege hiyo ilipata engine Failure mara baada ya kupaa.Uchunguzi bado unaendelea kufuatana na Tukio hilo.

Pia pongezi kwa Rubani aliyeweza kuokoa maisha ya abiria Hao na ndege kwa ujumla maana haijaharibika.Wengine wenye latest wataendelea kuchangia.
Aaa mi nili log in haraka haraka nikidhani bomba dear kumbe...any way pole sana waasirika mungu awape wepesi!
 
Ndege moja Aina ya Caravan yenye abiria 5 na rubani mmoja,Imelazimika kutua Kwa Dharura kwenye Shamba moja Pembeni Mwa kiwanja cha Arusha . Inasemekana ndege hiyo ilipata engine Failure mara baada ya kupaa.Uchunguzi bado unaendelea kufuatana na Tukio hilo.

Pia pongezi kwa Rubani aliyeweza kuokoa maisha ya abiria Hao na ndege kwa ujumla maana haijaharibika.Wengine wenye latest wataendelea kuchangia.
Huyo mwenye shamba kaneemeka !
 
Back
Top Bottom