Ajabu, mwizi kutoroka Mapinga kituo cha Polisi

Ajabu, mwizi kutoroka Mapinga kituo cha Polisi

mamsindo

Member
Joined
Jan 8, 2010
Posts
36
Reaction score
28
Tarehe 18 july majira ya saa 11.00 asubuhi mwizi alivunja dirisha na kuingia ndani kwa jirani zangu eneo la Kiharaka, Bagamoyo. Jirani walikuwa na mgeni wao kutoka Ulaya na siku hiyo hiyo muda mfupi kabla ya kuvunjiwa, mgeni alisafiri kwenda Tanga.

Mwizi aliingia kupitia dirisha la chumba kimoja cha kulala na akaelekea chumba kingine ambacho ndiyo mgeni wao alikuwa analala. Mwizi alivunja lock ya sanduku moja (Samsonite) kati ya masanduku mawili ya mgeni na kuanza kutoa vitu na kuchukua alivyotaka ikiwemo laptop.

Kufupisha habari,mwizi alikamatwa na alinusurika kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya mjumbe kuzuia watu wasimpige. Mjumbe alipiga simu polisi na wao wakafika kumchukua mwizi.

Jirani walipigiwa simu na wakarudi nyumbani ili kuona kilichotokea. Waliingia ndani kuangalia madhara.Kwa harakaka waliona uharibifu wa dirisha ambapo mwizi alikata baadhi ya nondo.

Pesa zilipotea, mkufu na pete ya dhahabu, sanduku Samsonite limeharibika,dirisha limeharibiwa,laptop ilipatikana. Kitu cha ajabu na ambacho hakiingii akilini kwa mtu mwenye akili timamu ni vipi mwizi atoroke kutoka mahabusu ya polisi?

Polisi wanapiga simu kabisa kusema ”Mwizi wenu ametoroka," mevunja dari! Kwa hali hii nani atakuwa na imani na polisi?

Sisi wananchi wa kiharaka hatuna imani na polisi wa Mapinga maana matukio ya wizi kwa sasa ni mengi mno.Si mchana wala si usiku. Tunahisi wezi wanashirikiana na polisi. Polisi inahitaji mabadiliko makubwa sana maana usalama wetu sisi raia upo mashakani.

Wanaohusika tafadhali fuatilieni hili.
 
Mapinga hadi serikali za mitaa ni sehemu ya mtandao wa Utapeli wa viwanja.

Kiwanja kimoja mtauziwa hata watu watano na serikali ya mtaa ikathibitisha mauzo.

Mapinga imeoza ni ya kusafishwa overall.
 
Wasaliana na uongozi wajuu

Hapo dawa tafuta namba ya DCO na hivi wanamuogopa mama lazima kieleweke
 
"Hilo nalo mkalifanyie kazi"
 
Back
Top Bottom