Mtumishi Wetu
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 5,711
- 1,914
Una maana hizo fedha analipwa DOWANS zinarudi tena CCM kuendeleza ufisadi wao??????????Dowans CCM ni kitu kimoja, kufanyia kampein au kulipa madeni ya kampeini. CDM komboa Mtanzania, tuandamane hakuna kulipa.Wacha Chenge ateme cheche huko Ulaya hatulipi. Tukimkamata akaingia kwenye anga zetu atatueleza, amuulize Mbaraka wa Misri!!!!!!!!!!!!Jamani msisahau kuwa hapa kinachotetewa ni pesa kwa manufaa ya CCM iliyowekwa madarakana kwa ufisadi wa aina hii.
Laana ya kuua inamtafuna anaweweseka, mpaka atubu maovu yake amrudie Mungu ndipo atapona!!!!!!!!!!!!You know what, the blood of those girls the wife killed that night will trouble him. Kwa sababu sasa anaongea hovyo kama mwedawazimu. Tena sijui kwa nini hajanyongwa mpaka sasa anatamba tuu.
Tena kweli anyongwe kabisa hata kama anatumia uchawi kuna siku tuu huyo Chenge
Jee kuna sababu yoyote ya maana kwa kutumia huduma ya mtu halafu usimlipe?
Kama ipi? Mbona juzi tumeona Kikwete akishinda kesi ya Mabilioni ya Rada, madudu yaliofanywa na Mkapa?
Nakumbuka Bunge lililopita, Mbunge mpya kwa tiketi ya cdm, Tundu Lissu, alipokuwa anajitafutia umaarufu Bungeni kwa kufanya u"tundu" na kuzua malumbano kwa kila hoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alisimama Chenge na kumpa Tundu hoja moja tuu ya kisheria ambayo ilimfanya Tundu kuwacha utundu wake wa kulumbana, kwani kwa pale ilidhihirika wazi kuwa Tundu ni katoto kwa Chenge kisheria. Nani anaekumbuka?
Kwa mantiki hiyo, ikiwa Chenge kasema fedha ya Dowans walipwe, basi ujuwe kaiona sheria kwa jicho la wazi na anajuwa kutokuwalipa Dowans kunaweza kuleta utata zaidi na kuliingiza Taifa kwenye utata zaidi, Jee, inawezekana kuwa hata Symbion hawatakubali kulipia mitambo ambayo bado ina deni?
Chenge anamatatizo, nawasiwas na uraia wake. Huyu bwana sio mzalendo kabisa. Kweli UFISADI IMANI YA HOVYO.
pascal njooBongolala, wakati nasubiri kulisoma hilo Nipashe, ningependa kusisitiza mahitaji ya kisheria na mahitaji halisi ni vitu viwili tofauti. Mahitaji ya kisheria ni laz`ima yatekelezwe no matter what, hata kama sio mahitaji halisi.
Tozo la Dowans lililotolewa na ICC ni hitaji la kisheria, kwa mujibu wa mkataba husika, uamuzi wa ICC ni uamuzi wa mwisho, haupingiwi na mahakama yoyote labda kufanyiwa mapitio na ICC yenyewe, hivyo kitendo cha kuusajili mahakama za nchini, ni kwa lengo la kuusajili uamuzi ule kwa utekelezaji tuu.
Siungi mkono tozo hiyo ya ICC kwasababu sio tozo halali, ila kisheria, maadamu wanasheria vichwa maji wetu waliukubali ule mkataba, na hivyo ndivyo mkataba unavyosema, then tozo hiyo imehalalishwa na mkataba mbovu ule, hivyo toso ile ni halali kisheria.
Nawaombeni wana jf na wananchi wote wa Tanzania, lazima tuukubali ukweli mchungu kwa kumeza kidonge kichungu cha tozo hii, tutatake tusitake, lazima tutalipa tuu, hatuna popote pa kutokea unless Tanzania kama nchi, tujitoe ICC na kuwafukuzia mbali hawa wanyonyaji wote wanaojiita wawekezaji wa kwendo makao n a mitaji yao, wakatumie fedha zao kutengeneza madini yao na sisi watuachie almasi zetu, Wasukuma tuzichezee bao, na dhahabu zetu tuziache humo humo ardhini, tubaki na umasikini wetu huku tumekalia malia zetu, kuliko kuwaruhusu wazipore kubadilishana na pipi huku wakituacha na umasini wetu palepale.
Huyu bwana damu yake ni ya kifisadi.Kama ufisadi ungewezekana kuwa inherited, tungeweza kusema ana genes za kifisadi.Katika kudhihirisha uswahiba na ufisadi wa mapacha watatu, Chenge amewasilisha pingamizi la kisheria kutetea DOWANS ilipwe na serikali ya Tanzania.
Source: Nipashe la leo
=============================================
DOCS:
More DOCS; DOWNLOAD THE ATTACHMENTS BELOW