Aiseeh! Washkaji pigeni simu kabla hamjaja maghettoni

Aiseeh! Washkaji pigeni simu kabla hamjaja maghettoni

instagram

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,118
Reaction score
4,879
Dah! yaani jioni nimepumzika zangu baada ya mishe zangu, nimefanya ka usafi kidogo ghetto nina msosi wangu ready kwenye microwave, soda yangu baridi kwenye friji nimeoga safi najiandaa nicheki muvi yangu huku nakula nilale mara paap mlango: "Ngo ngo ngoo" , mimi: "Nani?", msela: "Mimi hapa niko nje hapa".

Dah! Siyo kesi nasema, one time nafungua msela ananiambia ana ishu mbili za emergency. Ok namkaribisha ananieleza ishu za kichovu hazina hata uzito then namsikiliza kamaliza sijaona ishu ya maana yoyote ila msela ndo keshakaa na simu yake kaweka kwenye chaji yangu na ukimuona hapo sijui ndo katoka kwenye mazoezi sijui mihangaiko ananuka jasho ghetto lote halifai.

Yaani mtu kaniharibia mudi, hali ya hewa, na ndo kwanza katulia anacheki TV msosi unanisubiri kwenye microwave nashindwa nimuambiaje msela ili asepe yaani hana hata ratiba ya kuondoka na mimi nataka privacy ghetto kwangu.

Hivi inakuwaje mtu unaibuka tu kwa mtu bila mpangilio wala hata kupiga simu ili mtu ajue kwamba akukwepe vipi?
 
Nimekuelewa mkuu, muhimu mwambie direct tu kuwa siku nyingine atoe taarifa asije kiboya boya tu.

Ukimwambia kama muelewa na mstaarabu atakuelewa ila kama ni wale wazee wa kitonga mtaishia kugombana which is good kuliko kuwa na mwana mzigo.
 
Pivacy usifungue mlango,agonge akichoka atambae unakula bati tu.zamani pale mi na ma mwenye nyumba wangu baada kuchoka hodihodi nikamkabidhi funguo na kufuli.
Nikizama gheto anatia kufuli mda kuniamsha sa saba akileta lunch baas.
 
Huyo jamaa yupo humu jf?
hapo ujumbe hauwezi kumfika kama humu hayupo
BTW umeandika kama mwanamke, yaani mshikaji wako unamnanga huku badala umrekebishe kwa kumchana live na huo ndio ushikaji na uwana
 
Back
Top Bottom