Aisee kumiliki gari kumbe gharama hivi? Nimetumia 505,000/= kufanya service!!

Usiseme huwezi kupigwa kwakuwa wakati mnanunua mlikuwa wote. Mafundi wanajua wapi pa kupata kifaa kwa bei rahisi na wapi pa kupata kwa urahisi. Wengi wanakuwa na mawasiliano yao (maduka ya vifaa) kwa kazi zao za kila siku. So unaweza kupangwa kwamba kifaa ni 50k mkafika dukani ukaambiwa 55k. Ukipigwa 30k umepigwa parefu. N ukisema utafute vifaa mwenyewe utapigwa zaidi ya hapo.
Ukitafuta mwenyewe ukiwa huna papara hupigwi mkuu mie soea nanunua mwenyewe fundi anaenda funga tu kabla sijachukua naeza zunguka hata masaa matatu nafanisha bei hadi mtandaoni ndio nafanya uamuzi
 
Ukitafuta mwenyewe ukiwa huna papara hupigwi mkuu mie soea nanunua mwenyewe fundi anaenda funga tu kabla sijachukua naeza zunguka hata masaa matatu nafanisha bei hadi mtandaoni ndio nafanya uamuzi
Yani uzunguke masaa matatu ili uokoe elfukumi au 20?

Unaokoa 50 masaa 3 kazini kwako unapigwa laki 2 au zaidi.

Kujua sanaaa kuna leta uboya pia
 
Kwa masikitiko makubwa napenda kukwambia kuwa umepigwa kipigo cha mbwa koko.

1.Oil Seal wamelamba 10K inauzwa
25K
2.Break Pads 35K zile nzuri wamekula 10K
3.Engine oil lazima wamekuwekea 20W 50 maana ndio cheap ni 35K wamelamba 10K
4.Line brake haiwezi kuwa 40K wamekuchapa.
5.Hio hydraulic ni ya kitu gani ya kuuzwa 60K?
6.Gearbox mounting sina hakika.
7.Top engine mounting inaweza kuwa sawa maana mkoa tunapigwa 85-90K

Yani hao mafundi watakuwa wameenda na tabasamu la bashasha kwa wake zao maana kama ni wawili kila mmoja karudi sio chini ya 70K baada ya kugawana 100K na 50K waliokuosha dukani. Watakuwa wamefurahi sana pole sana mkuu! Siku ingine fanya utafiti madukani kwanza ukipewa listi.
Hydraulic ni ATF mzee mafundi wa mtaani ndo wanaita hivyo
 
Service imeshawahi kunigonga 1.2m na nilienda kufanya service ya kawaida tu gari ilikuwa normal kulikuwa na fault zilizoniwashia check engine. Mzee baki huko huko ukiwa na stress na pesa hivi vyuma vya mjerumani unaweza kujikuta umetumia milioni kwa ajili ya kuangaika kuzima zima vitaa vinavyowaka kwenye dashboad🤣🤣
 
Juzi fundi aliniuliza mara ya mwisho kufanya service gari langu. Nikamwambia mie tangu niagize nikaanza kutembea nayo sijawahi kufanya intensive service mpaka ipate tatizo ndio naileta kwako...
Hongera kwa kufanya service...japo kwenda na fundi si kigezo cha kutokupigwa....nasikitika kutangaza rasmi kuwa umepigwa kiasi..

Anyway, ndiyo kujifunza...ukishapata uzoefu nunua spea mwenyewe mpelekee fundi akufungie..
 
Juzi fundi aliniuliza mara ya mwisho kufanya service gari langu. Nikamwambia mie tangu niagize nikaanza kutembea nayo sijawahi kufanya intensive service mpaka ipate tatizo ndio naileta kwako...
Mwanamke mrembo naye gharama yake huwa hivyo ,ndio maana wanaume tunawasisitiza mtafute hela
 
Ukiwaachia gari kwenda kufata spare dukani wanatoa kifaa kizima, then wanakuchomekea kifaa kibovu, ukirudi unakutana na stori mpya tena

Mimi nawaitaga nyumbani na ni baada ya kufanya whole check up ya gari youtube, then namwambia tatizo..
Heheheh wee dada nomaa
Au fundi gari mwenyewe?.!!
 
Nayo sio mbaya

Mwenzio mwaka mpya nataka kuagiza gari mpya, but be4 this, hii miezi miwili iliyobaki nataka nikae na rafiki yangu pale NIT, anipige brush kuhusu kifaa cha gari kikiharibika, huu mtumba mpya ukiingia bongo nakuwa expert sikanyagi kwa fundi tena, zaidi ya kufungua nut na kupachika kifaa kipya
Nunua na overall kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom