Aisee kumiliki gari kumbe gharama hivi? Nimetumia 505,000/= kufanya service!!

Mlolongo

JF-Expert Member
Jul 4, 2019
3,271
5,892
Juzi fundi aliniuliza mara ya mwisho kufanya service gari langu. Nikamwambia mie tangu niagize nikaanza kutembea nayo sijawahi kufanya intensive service mpaka ipate tatizo ndio naileta kwako.

Akashangaa sana. Akasema kawaida unaponunua gari either kwa mtu au kutoka nje, kabla hujaanza kuzurura nalo lifanyie service kwanza. Bila kujali aliyekuaa nalo alifanyia service lini. Labda hiyo gari iwe brand new.

Basi nikamwambia kesho (ambayo ishakua jana) nitaileta tuifanyie service. Kesho yake mapema tu nikatoa gari nje, nikafungua boneti, cheki oil na maji kwenye rejeta. Maji nikaongeza kidogo.

Nikatimba kwa fundi wangu mzuri pale Sinza Palestina. Tukaanza kazi. Uzuri step zote nilikuepo. Fundi ana vijana wake wawili. Namie nikawa pemben nawapiga tafu.

Wanafungua hiki, wananiambia kazi yake na kama kiko sawa wanasema kiko sawa. Wanafungua kile, kama hakiko sawa wanasema boss inabidi tubadilishe hiki, kimeisha sana.

Anyway, jioni nakuja kupewa mchanganuo wa gharama aisee nikasema "Bhagoshaaaaa mweeeee".

Ukiona mtu anaendesha gari kali barabarani kila siku mwamkie " shikamoo". Kumiliki gari inabidi ujipange aisee. Unakuta kampira au kachuma kadogo tu kanauzwa 65,000/=. Au kale kamkanda ka kwenye Steering wheel kana bei kubwa hadi nikashangaa!

Mchanganuo wake:
Vifaa, Fluids = 405,000
Ufundi = 100,000
Tip = 0
Jumla = 505,000

Fundi alisema gharama za vifaa hatuwezi ku-negotiate maana tumevinunua namie nikiwa nashuhudia. Gharama za Ufundi ndio tunaweza ongea.

Hata hivo kutokana na nilivokua nawaona vijana wakizama chini ya uvungu wa gari, wanamwagikiwa na oil, wanachafuka kinoma, wanafungua nati zingine zimekazwa kinoma, sikuona haja ya kugalaliza hela ya Ufundi.

Labda tu, safari hii sijampa fundi ile "Tip" ambayo nishagamzoesha.

ADDITIVE POINT:
Kitendo cha mie kuwasaidia mafundi wakati wanafanya service ya babywoka yangu imenifanya nijifunze vitu vingi sana kuhusu gari. Yaani hapa nilipo naweza kufungua boneti nikakuelezea kazi ya kila kidude, kila waya, kila pipe, kila chuma.

Matatito mengine madogo madogo nitakua nayamaliza mwenyewe home. Uzuri Toolbox ninayo.

Sio unakua kama Extrovert hata Fog Light ikiungua lazima aende garage pale Majengo Moshi.

Yaani mtu kama mng'ato anamiliki gari kali, lakin yeye anachojua ni kuwasha na kuondoka tu. Hata ukimuuliza hivi ukipiga honi ikawa hailii hatua ya kwanza utafanyeje, hajui!!!

IMG_20200923_175308_8.jpg
 
Usiseme huwezi kupigwa kwakuwa wakati mnanunua mlikuwa wote. Mafundi wanajua wapi pa kupata kifaa kwa bei rahisi na wapi pa kupata kwa urahisi. Wengi wanakuwa na mawasiliano yao (maduka ya vifaa) kwa kazi zao za kila siku. So unaweza kupangwa kwamba kifaa ni 50k mkafika dukani ukaambiwa 55k. Ukipigwa 30k umepigwa parefu. N ukisema utafute vifaa mwenyewe utapigwa zaidi ya hapo.
 
Kwa masikitiko makubwa napenda kukwambia kuwa umepigwa kipigo cha mbwa koko.

1.Oil Seal wamelamba 10K inauzwa
25K
2.Break Pads 35K zile nzuri wamekula 10K
3.Engine oil lazima wamekuwekea 20W 50 maana ndio cheap ni 35K wamelamba 10K
4.Line brake haiwezi kuwa 40K wamekuchapa.
5.Hio hydraulic ni ya kitu gani ya kuuzwa 60K?
6.Gearbox mounting sina hakika.
7.Top engine mounting inaweza kuwa sawa maana mkoa tunapigwa 85-90K

Yani hao mafundi watakuwa wameenda na tabasamu la bashasha kwa wake zao maana kama ni wawili kila mmoja karudi sio chini ya 70K baada ya kugawana 100K na 50K waliokuosha dukani. Watakuwa wamefurahi sana pole sana mkuu! Siku ingine fanya utafiti madukani kwanza ukipewa listi.
 
Kwa masikitiko makubwa napenda kukwambia kuwa umepigwa kipigo cha mbwa koko.

1.Oil Seal wamelamba 10K inauzwa
25K
2.Break Pads 35K zile nzuri wamekula 10K
3.Engine oil lazima wamekuwekea 20W 50 maana ndio cheap ni 35K wamelamba 10K
4.Line brake haiwezi kuwa 40K wamekuchapa....
Hapo namba 5 ndio wamempiga vibaya mno
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom