Airtel yatosha wezi wakubwa

Pota

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
2,031
760
Wanajamvi naandika huu uzi nikiwa muhanga wa vifurushi vya airtel. kuan wanajf wataanza kusema nimetumwa na mitandao mingine...la hasha mi bado natumia airtel but lazima niseme kwani nimekanyagwa.
Mara nyingi nikitumia bando kwenye modem huwa naweka line kwenye simu ili nnitumie airtime, naomba ieleweke wazi kuwa huwa simalizi bando la internet japokuwa huwa sichunguzi sana. lililonisibu jana ni kuwa nimenunua bando la sh 999 nikapewa mb 250 airtime 40minutes nk.nikatumia internet na nikaweka kwenye simu line nikaangalia salio kukawa na airtime 40dkka,na 136mb.cha ajabu naangalia leo salio ili nitumie kwenye internet kukawa kumebaki 50kb, nilishikwa na butwaa...kwani sm yangu haina internet,muda wa kuexpire ulikuwa bado masaa manne.nimekwazika sana na hawa wa.senge.....sijui kwa nini wanatudanganya danganya na hivi vifurushi.
mods naomba msiniban kama nimetumia lugha mbaya ukizingatia sijawatus nyie incase...nilikwazika sana na hawa vichaa
 
Ripoti case yako TCRA may be they will give guidance!
 
Airtel ni mtwangio wangu lakini wanakera na vtu vingine wanavyovifanya makusudi.juz ijumaa best yangu mmoja mida ya jioni ameweka jero ili asubuh anunue bando!kwan ameikuta jero?mpaka leo
 
Hawa TCRA nadhani wapo kwenye paylol ya haya makampuni ya simu, mimi natumia airtel na huu ujambazi unafanyika, tangu walipoifuta ile bandle ya shilling 2500 per 400mb, basi sasa hivi ni wizi mtupu

Ukiweka modem ya tigo ndio chafya kabisa mtandao unakuwa slow sana, kwa kifupi hizi mb 50 za promo hazifai kabisa, na mfano huwa nikiweka bundle ya 24 hours ukidisconect usiku asubuhi upati net wakati yale masaa yanakuwa hayajatimia.

Sijui Watanzania ni idara ipi hatukamuliwi maana kila sekta tunakamuliwa na kuibiwa kimachomacho.
 
........yaaani utafikiri hizi bundle tuliwaomba. Vigezo waweke wenyewe kisha wanatuzunguuka nyuma kututia vidole
pathetic lunatic !
 
Mimi pia nimewah kununua unlimited ya masaa 24 but hata nusu siku haikufika! Ukiuliza eti bundle zimeisha. Sasa kwa nini uliita kifurushi cha mda? Hapa nlipo nimenunua cha wiki cha elfu 11,500 lakini najuta, spidi yake mwisho 70 kb per second, yani bora ila ya bure saa 6 usiku inafika mpka 1mb per second. Ukiwapigia customer care wanajeuri sana hawaskilizi mteja.
 
Ni wezi wakubwa ila naendeles kuwavumilia. Tokea huu mwezi uanze wakiwa wamepandisha gharama zao imekuwa kero. Nanunua bundle la shs. 5,999 napata muda wa maongezi, sms na 2GB kwa siku 7, cha ajabu inanikuta siku ya 7 Airtel Yatosha inaisha jioni kwenye 18:00hrs, alfajiri ya hiyo siku salio la bytes lote wanaondoa linakuwa 0Byte ila muda wa maongezi na sms unakuwepo. Nimeshawapigia simu kuhusu ili tatizo wanasema wamerekebisha lakini hakuna marekebisho yoyote.
 
wale wengine nao, wanakwambia nunu bundle ya dakika 40 mitandao yote !
Ukijiunga na kulipia, wanakiujulisha, dakika 20 yao, 20 mitandao mingine !
Hovyoo kabisa !
 
Bora na mm nimwage dukux2 langu leo, mm natumia kile kifurushi cha 1999 cha week. Wanakupa msg 700, call mnts 60 na bundle ya internet ambayo kwenye cm yaku siwezi kutumia, sasa tatizo langu ni pale nnapoamua kuongeza hela ili niweze kupiga cm nje ya nchi! Ukimaliza kuongea tu, lile bundle lako lote utakuta limeisha na ile hela uliyoweka inatumika kwa spidi ya ayabu hujawahi kuona. Sasa mtu nimejiunga asubuhi kifurushi cha wiki! Labda nimetumia msg 10 na 20 mnts za maongezi! Jioni naweka elfu 5 ili nipige cm nje, weeee wanalamba kila kitu! Imekaaje hii wenzangu?
 
Airtel Yatosha sitaki hata kuisikia tena......

waizi waizi sana,na ukipiga customer care
kila mtu atakupa jibu lake ni mkanganyiko tu....
 
Back
Top Bottom