Airtel wapandisha gharama

Aisee, Leo nimeshtushwa sana na bundle za Airtel. Nimezoea weka bundle za wiki kwa Tsh.6000 na zaidi ni hiyo 2GB.
Sasa Leo nakuta Tsh.6000 napata 500MB:A S 13: Jamani!!

Sasa basi kihesabu/Kiuchumi, 2GB kwa wiki ni sawa na 285mb kwa siku.:hand:
Ukiweka kila siku bundle ya Mb250 kwa Tsh.850, unakuwa palepale. Utatumia Tsh.5950 na utapata 1.75GB
Au weka kila siku bundle ya Mb300 kwa Tsh 1000, Utatumia Tsh.7000 na kupata 2.5GB.

Sawa na kusema:
Airtel wameongeza Shs. 1000 na kuongeza Mb100 au wamepunguza mb250 na kutoa Tsh.50.:A S 112:

Sasa basi waturudishie bundle yetu ya wiki kwa shs.7000 kwa 2.2GB, Tuwe pamoja. Hii itapunguza usumbufu tu. :sad:

Tuko sawasawa?
 

Mlitarajia nini kutoka kwa #DogoLao na #Haitoshi ?

Wenzao Vodacom ni #KilioBombastic !
 
Duh nimenunua juzi bundle imeisha cjui imeishaje
 
Duh nimenunua juzi bundle imeisha cjui imeishaje

unashangaa? tcra ndio kwanzaaaaaa wanachekelea minoti yao. nyie wenyewe si mliamini kwamba hao ndio baba lao na yatoshaaaaa? duuuh! pole weee! sasa wajua kwamba ni dogo lao na haitoshiiii? poleeee!
 

Madhara ya kutowajali watu wenye kipato cha chini!!!!!!
 
Madhara ya kutowajali watu wenye kipato cha chini!!!!!!

Wakati wa Nyerere walikuwa hawapo wenye vipatoo vya chini? tena tulikuwa masikini wa mwisho duniani na bei za kupiga simu ndio kama nilivyokuwekea. Enzi hizo ukiwa na simu ya nyumbani unaonekana wa maana kweli kweli. Leo mna neema hata wale wa kipato cha chini ya kima cha chini wana simu na wanadunda kama kawaida.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…