Airtel wapandisha gharama

haya makampuni ya Simu yote majizi tu, hawa Airtel nao wanaanza kujisahau wameona watu wamehama mitandao mingine, sasa wanajisahau.
 

Hebu nyambulisha, hizo dakika zipi ni za off-net na zipi ni za on-net au hizo dakika unapiga mtandao wowote?????
 
Mungu wangu ndo mapicha gani aya ameleta apa airtel yan me najiunga ya wik kwa dk 100 leo hakuna imebid nkajiunge ya dk40 kwa wik . Na naamini ntatuma sms zaid kuliko kupiga
 
hameni lakini huku voda msije wanatoa mb 100 kwa vifurushi vyote.
 
Pia wamekuja na 'system' inayokata 'more seconds' zaidi ya unazotumia. Mfano, Juzi nilipiga simu kwa sekunde 25, na salio langu likiwa sekunde 230. Baada ya kumaliza ikanijulisha nimebaki na sekunde 120. Watakuwa wameweka 'algorithm' inayoongeza sekunde wakijua ni vigumu watu kushtuka.

Suruhisho ni kuwa na chombo kingine cha CCC kwani TCRA-CCC imeshindwa kazi!
 

Hawa jamaa bado wako juu ukilinganisha na Tigo, ambao bado wanajipendelea katika vifurushi vyao, hasa vya Mini Kabang. Ukinunua kifurushi cha shilingi 599, unapewa dakika 14 za Tigo-Tigo, lakini dakika 6 tu kwenda mitandao mingine. Ujinga huu hakuna Airtel. Wewe unanunua kifurushi na unapiga mtandao wowote unaotaka. Pia unapojiunga na kifurushi cha Airtel unajulishwa muda wa mwisho wa kukitumia na kila unapomaliza kuzungumza unajulishwa umetumia sekunde ngapi na sekunde ngapi zimebaki.
 
Amarula _the spirit of Afrika
Wakat dunia ikiwa kwenye tikisiko kubwa la mamilion ya watanzania wanaburudka na Coca
Safari laga_urithi wa mtanzania.
 
Yote haha kwasababu ya kupanda kwa ghalama za umeme nahisi
 
Sasa mie nina hama kabisa kwenye mtandao huo kuna mtandao mmoja sms mwaka mzima bure,kazi yangu sms tu, net ndo hela ila sms bure mwaka mzima, no call sms onlly my future plan

Huo mtandao ni siri?
 

Vifurushi vya wiki je?
 
Ila bado wako chini, ngoja kesho nikapate line yao hawa VODA wanaua sana, Tigo ndo kabisa wanakupa gharama nafuu lakini ukipata net unanyoosha mikono kushukuru

Internet ya Tigo mi nafikiri haipo kwani hata whatapp huwa inafungua mara chache sana
 
Tutanunua vya wiki.
Yaani wamepandisha kwa lift wala sio ngazi!
 

Nakumbuka Tshs 999/= ilikua inanunua Dk 61 + 5,000 Sms + 1.5 Gb wiki chache tu zilizopita, leo kwa same price hatupata hata nusu ya ile package?

Halafu tunaambiwa Mfumuko wa bei umeshuka na Pato la Mtanzania limekua, mara sijui Uchumi nao umekua kwa mwaka
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…