Pole sana ndugu yangu jinsi Airtel walivyokufanyia,hata mimi kama wiki mbili hivi zimepita,niliweka salio la elfu mbili ili ninunue bando ya wiki,wakati nanunua bando,nikapata msg kuwa salio lako halitoshi,ha! Nikashoku,kwa nini wakati bando ya wiki.ni shilingi 1999 na mimi nimeweka 2000 !! Kuja kuangalia salio nikakuta salio ni.1750 tayari nimekatwa 350,nikasema potelea mbali haidhuru,nikaongeza 500 tena,kuja kununua bando nikapata msg tena kuwa salio halitoshi kujiunga,ha! Nikashoku tena,kulikoni! Nikakumbuka ahaa kuna kamchezo kale ka mabingwa,lakini mimi ckuwahi kujiunga na kamchezo hako,
Nikapiga cm huduma kwa wateza,nikampata dada mmoja,akaniuliza kama niliwahi kujiunga,nikamwambia hapana,akanipiga longolongo akaniacha kwenye mataa bila jibu,nikapiga tena,nikampata dada mwingine,naye hivyo hivyo,nikapiga tena,nikampata kaka mmoja,yeye ndio akaniambie ni kweli tulikuunganisha kwenye mchezo kwa makosa hivyo tutashughukia suala lako ndani ya masaa 24,kweli kesho yake nikaweka salio nikajiunga nokakuta wamenitoa, kwa hiyo AIRTEL waliniingiza kwenye mchezo kwa nguvu,na pesa walionikata walisema.watanirudishia,hawakurudisha hadi sasa,kweli hata mimi walinikera sana.