AIRTEL TRACE MUSIC STAR: Mayunga atoa wimbo wake na Akon - Please don't go away

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
image.jpeg

Huyu dogo alishinda tuzo ya "Airtel Talent" pale Nairobi Kenya na baadae akapata offer ya ku-record wimbo na Akon. Kabla ya hapo alikuwa ameimba na Mr Blue.

Kwa sasa "single" yake aliyomshirikisha Akon imetoka, ni wimbo mzuri, hakika umemvusha dogo toka hatua moja kwenda nyingine. Wimbo mzuri na unasikiliza.

"Don't Go Away" ndio habari ya town kwa sasa.

Hicho kubwagizo alichoanza nacho ni tune ya wimbo wa 'the lion sleeps tonight',wenye asili ya afrika kusini ulioitwa 'mbube' kwa kizulu na kutungwa na solomon linda mwaka 1939. Baada ya hapo wimbo huu uliimbwa na wasanii wengine mbalimbali duniani.
Kwa hiyo Mayunga hajaonesha originality yoyote.
 
Napendekeza huyu sanamu yake iwekwe pale mnazi mmoja palipo na mnara wa mashujaa, huo uliopo wang'oe tu!
 
Kwavyovyote utakuwa Team Diamond & Zari tu wewe!
Hicho kubwagizo alichoanza nacho ni tune ya wimbo wa 'the lion sleeps tonight',wenye asili ya afrika kusini ulioitwa 'mbube' kwa kizulu na kutungwa na solomon linda mwaka 1939. Baada ya hapo wimbo huu uliimbwa na wasanii wengine mbalimbali duniani.
Kwa hiyo Mayunga hajaonesha originality yoyote.
 
Mayunga mayunga mayunga mayunga, inasikika kwa mbaaaali. The song is very nice, very promising future for this kid of ours.
Tumsupport huyu
 
Hicho kubwagizo alichoanza nacho ni tune ya wimbo wa 'the lion sleeps tonight',wenye asili ya afrika kusini ulioitwa 'mbube' kwa kizulu na kutungwa na solomon linda mwaka 1939. Baada ya hapo wimbo huu uliimbwa na wasanii wengine mbalimbali duniani.
Kwa hiyo Mayunga hajaonesha originality yoyote.
Huu wimbo Mayunga ajaandika, yeye alienda kuimba tu.Muandishi wa huu wimbo ni AKON mwenyewe na ulichelewa kutoka kwasababu kuna vipande vya wimbo wametoa kwenye wimbo mwingine ikawalazimu kuomba kibali kutoka kwa mmiliki wa huo wimbo.
 
Ni jambo la kawaida kwenye biashara ya muziki, haipunguzi uwezo wa kijana wetu! Ni muimbaji mzuri na wimbo ni Mzuri kuliko.
Nimeona clip ya safari yake mpaka alivyorekodi huu wimbo unaona jinsi producer alivyokua na kazi rahisi, the boy is good
 
Back
Top Bottom